Aga Khan Hospital ni jipu hii nchi. Gharama za matibabu kubwa sana!

Issuna

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
3,168
7,513
Hospitali hii pamoja na kuendeshwa na shirika lisilo la Kiserikali, hivyo hailipi kodi, inatoza gharama kubwa katika matibabu yake.

Ingawa ni kweli kwamba ndio hospitali yenye vifaa bora pengine kuliko hospitali nyingine nyingi ukiiondoa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Pia ni Hospitali ambayo imekuwa na mchango mkubwa hasa kuokoa maisha ya wananchi.

Lakini kwa nini wasipokee wagonjwa wa NHIF? Ubaguzi huu wa nini?

Mhe. Rais aliwahi kuzungumza na Mtukufu Aga Khan alipotembelea hapa nchini, akawaambia waziangalie upya gharama zao za matibabu lakini bado ziko juu sana mpaka leo.

kwa mazungumzo haya ya WAZIRI MKUU sijui yatafua dafu au ndio yale yale ya Mkuu Rais wangu maana inakua kama tunawabembeleza vile wakati nchi yetu wenyewe ila sheria za matibabu wanatupangia wao.

pic+majaliwa.jpg

AGHAKAN mnaboa hata kama hamuelewi kiswahili ila ndio tusha waekea/wafungulia THREAD kukazia umbwiga wenu.
 
We hujui mwafrika hupambana na mwafrika mwenzake?

Suppose hiyo hospital ingekua ya mwafrika mwenzetu ingefungwa leo leo, ila kwakua ni mgeni wanamnyenyekea hata kama halipi kodi, waafrika hatupendani na serikali hua inaangalia wa kufanyiana nae vurugu.

Kuna waafrika wenzetu wanafungua hata vibanda vya biashara wanaandamwa na kodi mpaka wanafunga vibanda vyao maana profit hakuna tena.
 
Hizi gharama kwa agakhan no sahihi
Mfano dawa wanazotoa nyingi ni brand na huwa na bei kubwa ukilinganisha na za kawaida
Mfano
Ceftriaxone 1g ya ulaya kichupa kimoja kinaanzia 9000 wakati hizi za India zinazotumiwa kwa wingi mitaani hadi 700 unapata kariakoo, hivyo MTU atakaye chomwa hiyo dawa ya 9000 sindano 3 atatumia 27,000 wakati huyu wa dawa ya kawaida atatumia 2100
 
Pia kuhusu nhif wao catalogue ya bei za dawa nyingi huwa chini ukilinganisha na bei ya sako LA dawa za maana, hivyo ukisema agakhan wakupokee inamaa watakuwa wanakuwa huduma za juu wakati wao watalipwa kidogo na nhif, mfano utakuta dawa ya maana inagharama ya 20000 wao nhif wanaiwekea 7000 hivyo ili agakhan wakupokee itabidi either waue brand yao kwa kuanza kutoa huduma za kawaida kuendana na bei za nhif au waandae facility nyingine special kwa wateja wa nhif kama hospital zingine za maana wanavyofanya kuna hadi dirisha LA dawa kwa watu wa nhif na lingine limejitenga linaitwa private patients
 
Kuna ukweli ambao hua siku zote hausemwi na sijui kama ni bahati mbaya au ni vipi! Wakati tunailaumu Agakhan Hospital ambayo kimsingi ni taasisi binafsi na inachopata toka serikalini ni kusamehewa baadhi ya kodi katika baadhi ya maeneo kuna Hospitali kubwa za Taasisi za Kidini zinashangaza sana

Hizi hospitali za Taasisi za Dini kwanza zinanufaika na misamaha ya kodi kama ilivyo kwa Aga Khan lakini zenyewe zaidi ya hapo zinapokea ruzuku kubwa sana kutoka Serikalini ikiwa ni pamoja na kulipiwa mishahara watumishi wake(madaktari na wataalamu wengine}

Ajabu ni kwamba huduma katika hospitali hizo ni gharama kubwa sana hasa kwa wasio na bima za afya. Huwa mara chache wanatangaza matibabu bure kwa baadhi ya magonjwa kwa mfano fistula au macho na hii hua ni kwasababu maalum na ndio maana inapotokea hivyo inafanyika promo kubwa kwa hiyo miradi ya matibabu bure kwa magonjwa flaniflani., vinginevyo matibabu yanayohusu magonjwa mengine na hata vipimo vyake katika hospitali hizo ni ghali sana

Hospitali hizi katika baadhi ya maeneo zimepewa hadhi ya kua hospitali teule na zinahudumu kwa niaba ya taasisi za serikali jambo ambalo ni zuri lakini ingeangaliwa namna ya kuwapunguzia gharama wananchi hasa wasiokua na Bima

Tukumbuke kwamba kuna hospitali za jeshi ambazo serikali ingeweza kuzitumia kama hospitali za umma lakini ikaamua kushirikiana na taasisi za dini basi kuwe na usimamizi na ufatiliaji wa kuhakikisha bei za huduma zinakua zile ambazo wananchi wanaweza kuzimudu kwa kuzingatia ruzuku itolewayo na serikali ambayo ni kodi ya wananchi wote
 
Agakhan Hina matawi tabata segerea ,tandika mbezi ,kimara ,masaki ,bunju ,ukonga, mbagala yote hayo yanapokea Nhif z na service zote zinapatikana huko ww unakwama wapi

Inasemekana hivyo lakini nazani hapo kuna ubabaishaji fulani.

Kwanza hizo zahanati zao ulizotaja hutaweza kukuta daktari bingwa, nazani ni genera doctors tu.

Huduma huwa siyo ya kuridhisha kabisa huko
 
kwani bei za huduma ktk taasisi hizo za kidini zipoje chief? mfano kumuona daktari na kipimo kama cha malaria!
Kumuona daktari wa magonjwa ya kawaida sehemu nyingine hadi shilingi 10,000. kutegemea na hadhi ya hospitali. Kumuona daktari bingwa hadi 30,000.00

Kipimo cha malaria ni kati ya elfu tano na efu saba kama ilivyo kwa kipimo cha sukari
 
Kuna ukweli ambao hua siku zote hausemwi na sijui kama ni bahati mbaya au ni vipi! Wakati tunailaumu Agakhan Hospital ambayo kimsingi ni taasisi binafsi na inachopata toka serikalini ni kusamehewa baadhi ya kodi katika baadhi ya maeneo kuna Hospitali kubwa za Taasisi za Kidini zinashangaza sana

Hizi hospitali za Taasisi za Dini kwanza zinanufaika na misamaha ya kodi kama ilivyo kwa Aga Khan lakini zenyewe zaidi ya hapo zinapokea ruzuku kubwa sana kutoka Serikalini ikiwa ni pamoja na kulipiwa mishahara watumishi wake(madaktari na wataalamu wengine}

Ajabu ni kwamba huduma katika hospitali hizo ni gharama kubwa sana hasa kwa wasio na bima za afya. Huwa mara chache wanatangaza matibabu bure kwa baadhi ya magonjwa kwa mfano fistula au macho na hii hua ni kwasababu maalum na ndio maana inapotokea hivyo inafanyika promo kubwa kwa hiyo miradi ya matibabu bure kwa magonjwa flaniflani., vinginevyo matibabu yanayohusu magonjwa mengine na hata vipimo vyake katika hospitali hizo ni ghali sana

Hospitali hizi katika baadhi ya maeneo zimepewa hadhi ya kua hospitali teule na zinahudumu kwa niaba ya taasisi za serikali jambo ambalo ni zuri lakini ingeangaliwa namna ya kuwapunguzia gharama wananchi hasa wasiokua na Bima

Tukumbuke kwamba kuna hospitali za jeshi ambazo serikali ingeweza kuzitumia kama hospitali za umma lakini ikaamua kushirikiana na taasisi za dini basi kuwe na usimamizi na ufatiliaji wa kuhakikisha bei za huduma zinakua zile ambazo wananchi wanaweza kuzimudu kwa kuzingatia ruzuku itolewayo na serikali ambayo ni kodi ya wananchi wote
Haya unayoyasema hata Mr. President wakati ule alipowaalika viongozi wa dini ikulu aliwabia live bila kumumunya maneno.
 
kwa hospitali za serikali je?
Mwananyamala, Amana, Mnazi Mmoja haizidi elfu mbili kumuona daktari wa kawaida na kipimo kwa mfano cha malaria hakizidi 2000.
Hoja yangu ni kwamba hospitali zinazopata ruzuku zinatoza pesa sawa au zaidi ya zile hospitali za watu na mashirika binafsi ambazo hazipati ruzuku toka serikalini. Kwa hiyo ni vema kukawa na udhibiti wa bei za huduma kwa hospitali zote zinazopata ruzuku kutoka kwenye fedha za uma
 
hili kweli ni tatizo chief, kama wanapewa ruzuku na baadhi ya misamaha ya kodi hawapaswi kuwa na tozo kubwa kiasi hicho.

tulifikishe hili wizarani..
 
tatizo ni NHIF, wanataka unywe dawa za vichochoroni za bei chee ambazo zinatengenezwa kwa ajili ya 'wanyonge', sasa ukienda huko Aga khan unakutana na dawa wanazotumia mawaziri na mwenyekiti wa CCM na NHIF haitaki wewe 'myonge' uonje raha ya kutokua 'mnyonge' ili usije ukaanza kuwasumbua kwa kudai haki zako.
 
Back
Top Bottom