Ni heri kumshukuru Muumba wa nchi anayetukirimia kila iitwayo leo.
Andiko hili linahusu idara mbali mbali za afya,ni wazi kabisa afya ndio kila kitu,uchumi hauwezi kukua endapo afya ya binadamu haipo sawa.
Tukijikita zaidi kwenye idara ya udhibiti ubora wa madawa yanyotumika kila siku.
Katika nyanja hii ni wazi kabisa ya kwamba inabidi mfumo wa udhibiti madawa urekebishwe mfano,juzi Kati dawa aina ya MKONGO ilipigwa marufuku,ndyo labda walitafuta na kukuta Ina madhara.
Lakini Swali linaanzia hapa,je ni Nani alisajili hii dawa? Tuamini ya kwamba kuna ubadilifu au kufanya Mambo kwa mazoea?
Ni dawa iliyoanzia mtahani na imeishia mtaani,idara inayohusika wamekuja juu kuitoa sokoni lakini ukiangalia ni namba kubwa ya watu wametumia hii dawa Aina ya MKONGO.Tunapoteza taifa la baadae tunaharibu vijana wetu tunaharibu vizazi na tunaharibu uchumi ambapo badala ya kunufaika na dawa,vijana wengi wanaanza upya kutafuta matibabu ambayo haikuwa na ulazma wa kutumia hiyo dawa Kama ingefanyiwa utafiti wa kutosha.
Ni Jambo la kusikitisha na kuchukiza Sana kuona uzembe unaua vizazi,uzembe unaua taifa ambalo linaelekea uchumi wa Kati.
Idara ipo ili kusaidia kuondoa hadha kwa mwananchi,lakini pia hakuna uwazi katika kufanya maamuzi,kwanini hawatoi taarifa kwa mwananchi kwamba hiki kitu ni salama,labda utasikia vipodozi vimechomwa Moto,utasikia duka fulani limefungiwa,je,kwanini hawatoi taarifa kwa mwananchi kuhusu kipi kitumike na kisitumike?
Ni Jambo lenye kuleta taflani mtaani ambapo kitu kimezoeleka katika matumizi lakini idara inakuja kuzuia,inaleta wasiwasi na vifo visivyoelezeka,naomba tutambue ya kwamba kifo kinaanza kisaikolojia na zaidi kiafya.
Yaweza kuwa juu ya uzembe,njia za rushwa na kujilimbikizia mali,kwanini watanzania tuishi gizani?Kwanini tuharibiane soko ambalo tumelijenga wenyewe?Ni jambo la kupitia upya na kuliweka sawa.
Lakini pia,kuzorota kwa utendaji katika kazi Ni moja ya ukosefu wa maadili na uwajibikaji.Kila mtanzania ana haki ya kujua nini kinaendelea nchini bila kubaguliwa na mtu yeyote.
Mbona mikutano ya vyama,zihara za viongozi wa taifa inawekwa wazi lakini swala nyeti la afya linaenda kimaficho?
Kwanini bajeti ya nchi ipo wazi lakini katika ufumbuzi wa dawa mpya hakuna taarifa yoyote? Nini maana ya uongozi wa kitaaluma katika idara? Nini maana ya uwaibikaji Kama waliopo hawajali kuhusu hilo?
MAPENDEKEZO NA MAONI
1.Kabla ya dawa yoyote kuingizwa mtaani hasa dawa za tiba asili,kuwepo na tume ya kuifanyia utafiti wa kutosha na kuifanyia majaribio ili kuona uimara n ubora wa dawa kabla ya kutumiwa na binadamu.
2.TAKUKURU iingilie Kati kufatilia usajili wa tiba asili zote nchini ili kuangalia usajili wake umepitia hatua gani kabla ya kupelekwa kwa mwananchi.
3.Ziwepo hatua za kufata ili dawa kuwekwa hadharani,mfano mzuri ni kipindi cho COVID-19 yaani CORONA VIRUS, kurudi Cha homa Kali ya mapafu ambapo kila dawa ilikuwa inatangazwa kila hatua kuanzia uvumbuzi,inapofanyiwa utafiti inatangazwa na majaribio yanafanyika wazi-wazi na taarifa kumfikia kila mwananchi.
4.Tujaribu kufuata au kujifunza kutokana na nchi zilizoendelea,kwa maana hufata kila hatua ya kisayansi kabla ya kuruhusu matumizi ya kitu fulani hasa hasa Dawa. Na hizi taarifa hutangazwa kwenye vyombo vya habari kwa wananchi.
Tuwe wamoja kulinda afya zetu,Taifa Ni letu,Afya Ni zetu na Tanzania Ni Yetu.
AFYA NI YETU, TANZANIA NI YETU!.
Aljao
KAZI INAENDELEA.