Naomba kuuliza nini kinacho sababisha mwili kutokewa na majipu maana ninavyoongea saa hivi nina majipu mawili katika mwili wangu hivyo nilikua naomba kufahamu chanzo na tiba ya majipu?
Kama ni jipu,kwa maana ya jipu kweli,husababishwa na bakteria..
Wanaweza kuingia kwa kupenya ktk ngozi kupitia michubuko ama kupenya tu hata sehemu zisizo na michubuko..lakini pia unaweza ukawa na bakteria ndani ya damu ambapo wanaweza kusababisa jipu sehemu yoyote mwilini..
Kuhusu kujikinga ni changamoto kidogo..kama utaweza kukaa mbali na hawa bakteria ndio njia sahihi ya kujikinga..ila bahati mbaya sioni kama inawezekana..maana tunaishi na bakteria ktk mazingira yetu ya kila siku,hivyo, kujitenga nao haiwezekani..
Lakini hata hivyo,uimara wa kinga ya mwili ni factor muhimu..kutetereka kwa kinga mwilini kunaweka mwili wako ktk hatari ya kushambuliwa kirahisi, si kwa majipu tu,bali na magonjwa mengine..
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.