After all is said and done...

Hakuna masks za Mchina zenye ubora zaidi. Usitake kutwambia Marekani wanashindwa kutengeneza vitu vidogo kama mask. Tatizo ni mahitaji kuwa makubwa, hakuna motive nyingine tofauti na hiyo. Yani unataka kusema walizigombania kisa zina ubora?
Kwamba Marekani na Ufaransa wanashindwa tengeneza mask zenye ubora. Acha kumkuza Mchina kwa vitu vya kawaida kama hivi.

Nikikwambia unitajie product ambayo China anatengeneza kwa ubora utanitajia ipi. Mimi naweza kutaja makumi ya services au products ambazo Mchina hasogei kabisa mbele ya Mmarekani.

Uzi wako ulikoutoa wameeleza vizuri, wewe kwenye comments unaanza kuvuruga.
 
Reactions: Pep
..nahisi Marekani walikuwa na taarifa za ugonjwa huu hatari, isipokuwa wana Raisi mbovu asiyejua kuongoza nchi / dola.

..lingine ni kwamba Marekani akizama, China naye anazama.

..Marekani ndiyo watumiaji wakubwa wa bidhaa zinazozalishwa China.

..Sasa Marekani akianguka nchi gani itam-replace kama mtumiaji wa mkuu wa bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya China?

..baada ya ugonjwa huu hali ya uchumi ya dunia, na haswa nchi za DUNIA YA TATU, itakuwaje?

..Nimesikiliza Press Conf ya DG wa WHO na ameyaomba mashirika ya fedha ya kimataifa yafikirie hatua za kunusuru chumi za nchi za dunia ya tatu, na hatua hizo zihusishe debt relief.
 
Wengi wamechangia lakin nijuavyo kinachosukwa kitaonekana mapema sana, sio kweli kwamba mataifa haya na uzoefu wa majasusi wao kama CIA, Mossad, M16, na wengine wengi kamwe china angeweza cheza karata hii bila wao kung'amua...wengine wanaweza kusema mbona nao wanakufa kama walijua, lakini jua ili kumwathibu adui lazima utafute sababu ya binadamu kupata hasira, unazan baada ya hii corona kuisha ikajatokea sababu kwamba china ndio aliileta atapatwa na ninini? Magharibi wanaweza ishi bila mchina kabisa ila nikuulize china wanaweza? Magharibi wanaweza sema kwa sababu ya janga hili ni marufuku kushirikiana na china including africa na africa mkatii na atakae thubutu akaathibiwa ila mchina anaweza sema nchi yeyote isishirikiane na magharibi? Suala la mchina kukalia kiti cha u super power hizo ni ndoto za saa saba mchana sahauni kabisa abadan haitakaa ikatokea, kuna soo many things china is far away to archieve and it will take hundreds of years kufika ili itake kuwa super power

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchina product yake Inayo last long ni corona.

Namsifu mchina? Una wazimu.

Wewe unafikiri ni kwanini wanaziita โ€œcoronavirus masks from Chinaโ€ na siyo face masks?
 
Nchi za dunia ya tatu zitakuwa chali! Flat! Mambo mengi sana yatabadilika kiuchumi, kisiasa na kijamii vilevile.
 
Lazima tutafikia huko, after all is said and done, lazima kutakuwepo na power struggle upya duniani.
 
Na waliwambia Babu Trump kabisa Don't underestimate Beijing!!
Nina marafiki zaidi ya 30 wa china karibia ya wote husema huu ugonjwa hauta wasumbuwa huko kwenu!!
 
Dunia ina mengi china akisema kuanzia leo dawa ya cancer na ngoma na sijuwi kisukari nitatoa bure na unapona kabisa!! Ata pata wa kumfuata au ata kosa!!
USEMI mtu mzima akivuliwa nguo huchutama una maana nzuri sana!
 
Mchina product yake Inayo last long ni corona.

Namsifu mchina? Una wazimu.

Wewe unafikiri ni kwanini wanaziita โ€œcoronavirus masks from Chinaโ€ na siyo face masks?
Hii nayo ni point?

Nikiamua kuziita...
1. corona virus face mask
na mwingine akaziita
2. face mask
...utatoka na jina la kwanza ukilitumia kama uthibitisho wa hoja zako za kufikirika?

Hilo jina la kwanza wanalitumia kutofautisha aina za mask inayotajwa. Mtu anaweza nunua mask gulioni kwa ajili ya michezo ya mazingaombwe, nayo hii inaitwa mask. Mtu wa maabara anaweza nunua gas mask kwa ajili ya kujikinga na gas kama Chlorine.

Wewe unatumia "utumizi wa lugha" kujadili matukio na mahitaji ya kisayansi.
 
Pass.
 
Na waliwambia Babu Trump kabisa Don't underestimate Beijing!!
Nina marafiki zaidi ya 30 wa china karibia ya wote husema huu ugonjwa hauta wasumbuwa huko kwenu!!
Siwezi kudharau kauli zao. Ila ngoja muda kidogo upite. Kama ni kweli hii inazidi kuimarisha hoja iliyopo mezani.
 
Nakubaliana NA wewe,mchina kwasasa hawezi fanya BIASHARA na yeyote coz kuna lockdown. Pia kua tarifa niliona Aljazeera Spain na German wamezikataa mask za misada toka uchina kwasababu ya kutokithi viwango vya EU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu na Mimi niwaze tu kivyangu
Kama umeweka maili zote hizo kutoka Wuhan kwenda kwenye miji yote
Basi hawa wadudu walibebwa na wachina wenye kinga na kupeleka na kusambaza kwenye baadhi ya miji mikubwa
Jamani hapa nawaza tu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Na nchi za ulaya zinapanga kwenda kumalizia ligi zao za mpira huko china

Sent from my vivo X21 using Tapatalk
 
Swala kama US Walikua wanajua kuhusiana na Huu Ugonjwa Inaweza Ikawa Siokweli Maana wasingekua tayari Kuutoa kafara Uchumi wao unaopitia kipindi kigumu kwa sasa Kuhusiana na Donald Turampet Yule Kenge Hajawahi Kua Naakili Toka Anazaliwa mpaka hapa alipofikia

Sent using My COVID-19
 

..sidhani kama Bill Clinton, George Bush, au Barack Obama, wangezembea huku wanaona China kunawaka moto. Lazima wangejiandaa na kuchukua hatua za tahadhari.

..Trump yeye alivyoona China alidhani janga hilo haliwezi kuhamia Marekani, na yeye kwa akili na uzoefu wake vinamtuma kuonyesha " a good picture " about America kuliko uhalisia. Yeye anataka stock markets zisomeke vizuri kila wakati hivyo yuko radhi kuongopa na kuficha ukweli.

..Na Trump alipoingia madarakani akaanza kupiga panga fedha zinazokuwa allocated kwa taasisi kama NIH[ national institute of health] na CDC [ center for disease control] . Taasisi hizo ni muhimu sana ktk kufanya utafiti na uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ