After all is said and done...

inaonekana usa anatafuta vifaa popote pale duniani na siyo china tu ukumbuke hata misri, italy walipeleka mask za msaada wuhanchina mwezi February.
 
Mkuu China amejipakazia kidogo tu ili kuondoa lawama.

Maana inaonekana walifahamu athari za kirusi hicho kabla hakijasambaa. Wengine duniani waliona ni kama mafua tu, hadi walipoanza kudondoka kama nzi.

Au pia unataka kusema ingeuwa watu zaidi kama ingeanzia marekani au Uingereza, Italy na Uhispania?
 
Hatari sana hii kitu, kama dunia imehamia kwenye bio warfare

Sent from ONEPLUS 5T using Tapatalk
 
Very well said mkuu. Ndo ukweli wenyewe huo.

Haiwezekani eti iwe bahati mbaya mchina ndo mnufaika mkuu wa gonjwa hili liloanzia kwake. Sema ni mjanja amejitapakazia kidogo tu ili anuke kama wengine. Lakini kiukweli yeye hana huo mgogoro! Hadi mataifa ya magharibi yakawa yanasema wanaficha takwimu za ukweli. Sababu haiwezekani gonjwa lianzie huko halafu viama kwingine huko! Na wao eti kuwa wamejindaa vibaya mno.

ngumu kumesa!
 
Hatari sana hii kitu, kama dunia imehamia kwenye bio warfare

Sent from ONEPLUS 5T using Tapatalk
Ndiyo hivyo mkuu, wamepigana sana cyber warfare lakini ni watu hawajui tu. Wako kwenye vita kitambo tu, sema silaha hazitumiki.

Mkuu mmarekani ana military base kila kona ya dunia, lakini mchina ni wakandarasi na ma engineers nk wako kila kona. Na hao raia wao.
 
Ndiyo mkuu!! Kwa jamii za kiliberali za Ulaya na Marekani kama ungeanzia huko huenda ingekuwa balaa zaidi maana sidhani kama raia wao na wanasiasa wa huko wangekubali hatua kali za udhibiti kama China.

Na pia usisahau hizi hatua walizochukua sasa za kufunga shughuli za kiuchumi na baadhi ya miji wameiga kutoka China baada ya kuona mafanikio yaliyopatikana huko.

Kuhusu China kufahamu athari mapema hata Marekani na Ulaya kwa wataalamu walionao lazima walifahamu ila walizembea au hawakuzipa uzito unaostahili kwa kuhofia kuzua taharuki kwa raia wao na kuharibu uchumi wao.

Mataifa ya Ulaya na Marekani hawawezi kukwepa lawama ya uzembe kwa kuchelewa kuchukua hatua kali za udhibiti mapema wakati maambukizi yalipokuwa machache.
 
Sasa West wao si wanapambana na Tanzania eti kuinyima mkopo WB watakuwa na mda wa kuwaza kutengeneza masks. ha ha ha ha. Wacha waendelee kupambana na petty things kama kumzuia gavana wa dar es salaam kuwatembelea.
 

Tatizo la marekani ni moja tu, they want to be everywhere all the times. Na watapasuka msamba tu, their days are numbered.
 
Mkuu, dunia hasa nchi za Magharibi zishafahamu kwamba madhara gani yanawezatokea endapo hatari ya milipuko mikubwa ya magonjwa itaanzia Uchina. Historia inatufundisha kwamba endapo Uchina itapata ugonjwa hatari basi Ulaya haiwezi kupona kwasababu wameunganishwa na biashara (The Silk Road). Ugonjwa wa Tauni (Bubonic Plague) ulianza Uchina lakini ukafika Ulaya na kuua mamilioni, ugonjwa wa mafua ya uhispania (Spanish Flu) imegundulika ulianzia Uchina na ugonjwa wa SARS nao ulianzia Uchina.

Yote haya yalianzia Uchina kusambaa duniania kote kwasababu ya umuhimu wa Uchina kwenye biashara ya dunia. Sasa leo hii Uchina ndiyo nchi ya kwanza kuwa na viwanda (Factory of the world), nchi ya kwanza kuuza bidhaa nyingi duniani (Leading Exporter of Merchandise) na Mnunuzi mkubwa wa bidhaa (Second Largest Importer ) hivyo haepukiki. Nchi adui wa Uchina akianzisha vita ya kibaolojia basi hata yeye hatapona lakini hata Uchina akiataka apigane vita ya kibaolojia hana haja ya kupiga kwa adui, anaweza kuanzishia kwake na maadui wakaufuata kwa hamu.

Nakumbuka huu ugonjwa unapoanza kuna mzee mmoja ni mwalimu wangu niliwasiliana naye ndiyo akaniambia niyaangalie mambo kwa mapana yake. Baada ya miezi kama miwili nakuta kila alichoniambia kinatokea hasa hasa kuhusu Uchina kuhusika. Hatuwezi kusema kwamba ni Uchina lakini pia hatuwezi kukataa kwamba siyo yeye. Muda tu ndiyi utasema kweli.
 
Ukiona mchezaji ameacha league kuu na kuanza kucheza mechi za mchangani ujue lime time yake ndo inaikwisha hivyo. Kutoka superpower hadi kufikia kutisha watu kama makonda, jua tu hapo kwisha habari yake , anachokuwa anajaribu kufanya ni to make himself big. Na ndiyo falsafa ya mchezaji kurudi mchangani.
Sahivi China financially strong, and Russia militarily very powerful than ever before.
 
athari zijazo baada ya hii Corona zinaweza kuwa mbaya kuliko Corona yenyewe..
Revenge inayokuja kwa ujinga wa China inaweza kuwa kali kuliko ile aliyopigwa the the king of the pacific..

Dunia ilishatoka kwenye haya maujinga kuanzia 1970's kushuka chini, Mchina anataka kuirudisha dunia huko. Bila shaka atapata akitakacho mwisho wa siku na kuanzia hapo dunia itakuwa kuoneshana umwamba mpaka apatikane mwamba mwingine.. Hii alama ya USA kurudisha raia wake USA ni ishara ya revenge inakuja..
 
Well articulated analysis of the conspiracy theories related to COVID-19.
 
Ukisoma michango ya watanzania wa humu, unaweza sema wanajua kila kitu.
Kumbe kila mtu anaandika ili aonekana anajua kumshinda mwenzake.

Mnayoyaongea ni sawa na kuwa na dawa na kuua watu wote duniani ili ubaki mwenyewe ukimiliki mali[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha ha ha
 
China mwaka 2018 na 2019 walitengeneza zaidi ya nusu ya masks zilizotengenezwa duniani.
Wala hazina ubora huo unaousema. Spain, Italy na Turkey washasema hizo masks zina ubora hafifu. Spain ilidai testing kits kutoka China zina ufanisi wa 30% tu.

Factors nyingine zinazowafanya China wauze sana masks ni gharama ndogo za uzalishaji hivo hazina bei sana. Pia ugonjwa ulianzia kwao hivo walizalisha masks kwa wingi na miundombinu ya masks iiliongezwa maradufu.
 
Marekani kukopa NATO tena au hujui maana ya NATO?

Marekani kukopa ECB wakati WB ipo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ikigundulika kafanya CHINA Unahisi watamfanza nn maana uwezo wakumpiga kijeshi hawana nawala hawatakaa wajaribu labda nawao waingie maabara tu labda ila hakuna wanaloweza kumfanza kiukweli

Sent using My COVID-19
 
Umefuatilia hiyo story ya marekani na ufaransa kupigana bao kwenye face mask za coronavirus? Mmarekani alipanda dau airport akalipa bei mara mbili mzigo ukageuza safari kwenda USA. Ina maana zina ubora zaidi mbali na kuwa kuna ukosefu kutokana na mahitaji kuwa makubwa zaidi.
 
Marekani kukopa NATO tena au hujui maana ya NATO?

Marekani kukopa ECB wakati WB ipo.



Sent using Jamii Forums mobile app
NATO wanashirikiana kwenye mambo ya ki ulinzi na wanasaidiana kwenye migogoro nk.

Ndiyo, mataifa Huwa yanakopeshana we vipi? Unaniambia sijui maana ya NTO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ