Afrika shoka lilikosa makali

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
32,174
75,567
Uchungu wa mimba kwa mama ndio kama upendo wa mama kwa mtoto lkn Afrika hilo limepotea!

Uchungu wa Afrika ulikuwa ktk kupata uhuru lkn ni kama yowe lililopita bila kujibiwa!
Baada ya kupata tulichokitaka tumeshindwa kukitumia ipasavyo,njiti iliyowashwa imeishia patupu.

uzandiki na unafki uliopo unatula bila haya,nguvu ya mababu imetokomea kwa wafitini unafikiri ile mijitu myeupe itaacha kutudhihaki..?

lile shipa la aibu limetukatika! yote twaona shwari lkn kiukweli ni shwari lenye tabu la aina yake.

Bora ingekuwa mtoto asieelewa chochote lkn la hasha! toto hili jeusi linaelewa nakujua kuwa kuna hili na lile,kibaya zaidi wale ndege wakaao juu yake wanajaza yao tu! aaaaahh! na wamepita ktk msasa wa ubongo au ni uongo..? lkn si uongo maana wanapita na magamba.

he he! mbaya sana kupigania pigano lisilo na taji ila kwetu ndio hatutaki kuvaa taji ajabu ya karne..

Uhuru uso nuru

 
nyimbo nyingine hii hapa, tuimbe sote kwa sauti ya chini

1: Afrika nakutamani

Nikikumbuka sifa zako

Ingawa niko continent la mbali

Furaha haiishi moyoni


2: Nilihadisiwa na baba yangu

Kwamba kuna mavuno mengi

Samaki wa kwetu wanono

Si kama wa hapa America


CHORUS

Sina budi kukumbuka

Afrika nakutamani Sana

Afrika nakutamani
 
nyimbo nyingine hii hapa, tuimbe sote kwa sauti ya chini

1: Afrika nakutamani

Nikikumbuka sifa zako

Ingawa niko continent la mbali

Furaha haiishi moyoni


2: Nilihadisiwa na baba yangu

Kwamba kuna mavuno mengi

Samaki wa kwetu wanono

Si kama wa hapa America


CHORUS

Sina budi kukumbuka

Afrika nakutamani Sana

Afrika nakutamani
ha ha! Hilo lapili mmmh! Mavuno lkn njaa tunayo si haba!
Samaki wapo lkn bei sisemi kwa maana tunawaharamu sie wenyewe kwa sumu na mabomu! Njoo tupigane vita kutetea DINI toka mbali!
 
ha ha! Hilo lapili mmmh! Mavuno lkn njaa tunayo si haba!
Samaki wapo lkn bei sisemi kwa maana tunawaharamu sie wenyewe kwa sumu na mabomu! Njoo tupigane vita kutetea DINI toka mbali!
imba kwa sauti ya chini mkuu
 
Back
Top Bottom