Afrika na changamoto ya mifumo ya utawala

Afrika na changamoto ya mifumo ya utawala

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
501
Reaction score
1,214
Moja ya changamoto kubwa sana tuliyonayo hapa barani Afrika, ni nchi nyingi za Afrika kuwa na mifumo ya utawala inayotoa MAMLAKA MAKUBWA SANA KWA MTU/ TAASISI MOJA.

MAMLAKA MAKUBWA SANA ambayo yanaweza kuamua hatma ya maisha yako na
familia yako kwa ujumla.

Watu wengi kwa kutambua hilo, tunakuwa kwenye nafasi ya kutokusema ukweli au kutoa ushauri wa ukweli unaotaka ndani ya mioyo yetu kwa manufaa ya jamii zetu zinazotuzunguka.

Tunatumia muda mwingi sana KUPAMBA, KUSIFIA na KUPONGEZA MAMLAKA HIYO, kwa lengo moja tu la kukidhi matumbo yetu na matakwa yetu binafsi.

Ndio maana sio ajabu sana kwa Afrika, inapotokea mtu huyo kupoteza MAMLAKA hayo kwa sababu yeyote ile, watu wale wale waliokuwa wanasifu na kupongeza ndio hao hao wanakuwa watu wa kwanza kukosoa na wakati mwingine kutoa maneno ya Kashfa dhidi ya iliyokuwa mamlaka hiyo.

Kwa sababu watu wanakuwa hawawezi kusema ukweli kwa hofu ya kuudhi MAMLAKA, hivyo kuwa na hofu ya kupoteza FURSA.

Binafsi naamini kwa sasa, umefika wakati kwa nchi zetu za kiafrika, kurekebisha mifumo yetu ya utawala.

Tuwe na mifumo ya utawala itakayotoa fursa kwa watu/ wananchi/ viongozi kutoa mawazo na ushauri wao kwa ukweli bila unafiki na kujipendekeza kwa MAMLAKA.

Hii inaweza kutusaidia kututoa hapa tulipo sasa.

Mungu ibariki Afrika.
 
Back
Top Bottom