Afrika Kusini ni mojawapo ya nchi zilizoendelea kwa sekta ya viwanda duniani. Kwa ninavyofahamu miaka ya nyuma vijana wengi walikuwa wanakwenda tafuta ajira huko. Naomba uliza je kwa sasa nafasi za ajira iko vipi? Zipo au hazipo,je kuna wanaokwenda tafuta ajira bado ?
Wapo wengi wanaokwenda kutafuta ajira S.A ila wanachokipata ni Umauti.....wanauliwa sana na vijana wa S.A wavivu kufanya kazi wakiona mgeni anafanikiwa kwa kuchapa kazi kwa bidii wanampiga chuma!!
Sio sehemu nzuri kwenda, nimeishi huko miaka kadhaa nikaona hakuna dili nimerudi bongo mambo tambarare, nakushauri komaa hapa hapa Bongo opportunities zipo nyingi sana mkubwa.
Sio sehemu nzuri kwenda, nimeishi huko miaka kadhaa nikaona hakuna dili nimerudi bongo mambo tambarare, nakushauri komaa hapa hapa Bongo opportunities zipo nyingi sana mkubwa.