Afrika: Huku China kule Marekani

Afrika: Huku China kule Marekani

NG'UNDA

New Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
3
Reaction score
0
Ni ukweli usiopingika kuwa sasa bara la Afrika limewekwa kati na mataifa makubwa mawili duniani yenye sera na mitizamo inayotofautiana kwa kiwango kikubwa lakini wakiwa na malengo yanayofanana 'Uchina na Marekani'

Marekani imewaita viongozi wa afrika ili kujiweka sawa na kuendelea kujihakikishia ushawishi katika bara hili hasa baada ya kushuhudia Uchina ikijitutumua na kujipanua kiushawishi hasa katika sekta ya uwekezaji, kitendo ambacho ni dhahiri kinahatarisha Maslahi mapana ya Marekani kwa Afrika.

Mataifa haya yote yanapigania fursa za kuimarisha uchumi wao kupitia afrika, jambo moja ni kwamba wote wanaihakikishia afrika maendeleo kupitia sekta ya uwekezaji na misaada ya kimaendeleo.

Swali ni je Afrika inaweza kupenya katikati ya mpambano huu wa mataifa makubwa na kuibuka na maendeleo yenye uchumi imara?

Kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru tumepokea misaada ya kimaendeleo takribani USD trilioni 1 na zaidi lakini tumeshindwa kuendelea, Ni kwa kiwango gani mpango huu wa sasa kutoka kwa watu wale wale hasa nchi za magharibi unatuhakikishia sasa kuwa tutaendelea?

Kama Obama ameweza kuwaita kujadili na kusaini mikataba mbalimbali inayohusu maendeleo na rasilimali zetu za afrika, ni nini hasa kimewashinda viongozi wetu wa Afrika kukaa chini kwa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana na kuzi utilize rasilimali zilizopo hapa nyumbani kwa maendeleo ya afrika na hatimaye kuliondoa bara letu kwenye makucha ya utegemezi wa misaada?

Naiwazia Afrika, labda tusaidiane kutafakari.
 
Taizo ni masilai binafsi na tamaa na usaliti wa hawa viongozi wetu na hii haitaondoka hadi kiama kifike hapa duniani na kama msimamo wa wana afrika basi ni domo tuu na mashairi ya kumtitea mnyonge kumbe ni uzandik wa mwafirica
 
Viongozi wa africa wanapelekwa kama kondoo. Hawajielewi
 
tatizo ni kwamba hawajui hata kwenye ngumi kuna heavyweight (US, China etc), middleweight na uzito wa unyonya (Tz included)
sasa pambanisha heavy weight and feather weight uone matokeo yake.
 
tatizo ni uongozi wetu ,kila kitu kinaanzia kwa uongozi mbovu ndio maana inaleta shida kuendelea
 
Kuna tetesi kwamba marais na mawaziri wakuu wote wa Ulaya na Marekani wataitwa Chamwino (Dodoma, Makao Makuu ya nchi) kabla ya Krismasi. Asiyehudhuria automatically atakuwa amejitenga mwenyewe na Tanzania.
 
Back
Top Bottom