post yako imenikumbusha data niliyopewa na jamaa yanguanafanyia kazi mgodini geita.
alinambia kila siku ya Jumanne NA alhamisi, GEITA GOLD MINING(GGM) wanazalisha tofali 400 kwa siku hivyo kuzalisha tofali 800 kwa wiki na kwa siku 104 za mwaka, wanazalisha tofali 83,200.
Kila tofari ina uzito wa gramu 12,000
kila gramu moja ni tsh.65,000 kwa soko la ndani hapo hujapeleka ulaya wanakohitaji dhahabu kama binadamu anavyohitaji uhai/pumzi.
ukizidisha 83,200x12,000g=998,400,000grams kwa mwaka.
ukichukua grams 998,400,000x65,000=64,896,000,000,000/= pesa za kitanzania. mie sijui ni sh. ngapi kuzitamka, mtanisaidia.
ukikonvert kwa dolaa roughfly 1650 ie. 64,896,000,000,000/1650=3,933,090,909.909....USD, mtaniambia zinasomekaje kwa kiswahili.
USD 3,933,090,909.9
Watu wa kodi mje mtwambie tunapata kiasi gani kwa mgodi mmoja, kwa hesabu hiyo, hatujagusa migodi mingine iliyozagaa tanzania nzima.
Ni wazi kuwa, sisi ni matajiri, ila tumefukarishwa na CCM kwa sera zao mbovu, sheria dhaifu na viongozi waliotelekeza uzalendo wakaingia kujitajirisha wao wenyewe.
Kwa hesabu hii ya USD 3,933,090,909.91, nadhani zimezidi USD 102 million, 182.401 million na 1,706.38 walizojigamba kukwapua na kuwakumbusha TRA wana kazi ya kufanya .