Kuwa colonized ni kuwa fully chini ya Mamlaka ya nchi nyingine.
Hicho sicho ninachojaribu kumaanisha hapo. Mimi ningetamani Africa iendeshwe kama Kampuni ambapo Manager atasimamia
mambo yote mpaka ya kiutawala kama Muajiriwa, akimaliza muda wake anakuja mwingine.
Kampuni itakuwa na idara zake,nazo zitasimamiwa na Mameneja wenye taaluma husika,mfano Idara ya Nishati atakaa Mtaalamu wa Nishati n.k.
Rasilimali zote za nchi zitasimamiwa na kila baada ya muda tuliokubaliana Wananchi tutasomewa mapato na Matumizi.
Meneja na Wasaidizi wake wataishia kwenye mishahara yao tuliyokubaliana na Watakaguliwa na Kampuni za kimataifa zinazoaminika.
Waafrika kiasili si Wanufaishaji wa wengine,na ni limbukeni wa mali,uchoyo na tamaa ya kila mmoja kumzidi Mwenzake ndio tunaona ni maisha.Angalia hata Weusi wenzetu nje ya Africa,Haiti au Jamaica tatizo ni hilo hilo.
Nchi zinatengeneza "untouchables" wanakuwa na nguvu kiasi kwamba walio wengi wanabaki kusubiri huruma ya Viongozi ili hali tuna rasilimali lukuki.