WanaJF naomba msinishangae kuuliza swali hili kwani nimejifikiria mno na kutopata jibu. Huyu kaajiriwa na TFF kama afisa habari wake sasa kuongozana na timu ya taifa ambayo tena inaweka kambi nchini Sudan na kujifanya kuwa msemaji wake hii inanitatiza mno. Timu ya taifa ina kocha, msaidizi wake, manager n.k. hao wanatosha kutupa habari ya maendeleo ya timu yetu ikiwa ugenini. Hapa nchini pana mambo mengi tuu yanayotaka ufafanuzi toka TFF ikiwa ni pamoja na Uchaguzi mkuu, sakata la COREFA na ligi (wanayoiita) ya mabigwa inayoendelea nchini, yeye kaongozana na timu kwenda Morocco tena ikiweka kambi Sudan hapa pana ulaji tuu na si kingine.