Afisa elimu na mkuu wa wilaya Bukoba vijijini angalieni hili!!

kifuba

Member
May 27, 2013
49
39
Afisa elimu, mkuu wa wilaya na mashirika yanayojihusisha na haki za binadamu wilayani Bukoba vijijini msikilizeni na msaidieni mama wa mwanafunzi Anitha Adolph, darasa la sita katika shule ya msingi Karonge ambaye amepigwa na kuumizwa na mwalimu mmoja shule hapo aitwaye Nadhir kiasi cha kupatwa na hitilafu katika ubongo wake, mama yake ambaye yuko peke yake (single parent) amejaribu kufuatilia angalau huyo mwalimu aliyemuumiza alipie matibabu lakini uongozi wa shule ulimuita badala ya kumsaidia ukamwambia hawezi kusaidiwa kwa vile itakuwa kila anayepatwa na matatizo kama hayo anakuja kuomba msaada. Pia jana alienda kwa mkuu wa wilaya ili angalau apate msaada kilichofanyika huyo mama aliishia mapokezi na kupewa barua ya kuchangisha (harambee) kwa ajili ya matibabu ya mwanae, mtoto hawezi kutembea mpaka ashirikiriwe na mwalimu aliyehusika hajawajibishwa kwa lolote japo matibabu ya huyo mtoto. Ngazi zinazohusika hapo Bukoba msaidieni huyo mama maana sio mzoefu wa kufuatilia mambo ya kiofisi
Asanteni
 
Back
Top Bottom