Afisa Elimu ( msingi) Nyamagana anadumaza Elimu

serengo

JF-Expert Member
Jul 30, 2013
483
351
Kumekuwepo na Tabia ya kuwashusha vyeo wakuu Wa shule bila kufuata taratibu za kazi, mfano Mwalimu anapewa ukuu January halafu February anavuliwa madaraka huo ni uonevu Wa hali ya juu maana sababu zinazotolewa na ofisi ya Afisa elimu za kuwavua madaraka walimu ni kama zifuatazo.

I.Shule kutofanya vizuri kwenye mitihani?je January hadi February ni mtihani gani unafanyika na kiwe kigezo cha kumvua Mwl mkuu madaraka, inamaana kukaa pale kwa mwezi 1 ameharibu taaruma au mnatafutia magepu watu wenu?

ii. Sababu ya Pili wanayotumia :Mwl mkuu kutowaajibisha walimu wanaochelewa? Je ww kama Afisa elimu umeshakuja kukagua daftari LA mahudhulio ukatoa karipio,na wanafanya hivyo bila kujiridhisha ila kwa kupelekewa maneno ya kiongo na waratibu elimu Kata ili watu wao waweze pata nafasi hizo.

Afisa elimu anasimamisha walimu wakuu bila kufanya ukaguzi wowote, bila barua yeyote mfano barua ya onyo.

Walimu wakuu kwa sasa wilayani nyamagana wanakaa kwa Kusubili zamu tu ya nani anafuata.

Wito ninaomba idara ya Elimu mkoa Wa Mwanza Wamwangalie Afisa elimu ( Msingi) Wilaya ya nyamagana kwa jicho LA tatu, matatizo yamekuwa mengi mno.
 
Back
Top Bottom