AFCON (u17)-2017 Gabon: Serengeti boys special thread

keydu

Senior Member
Jan 3, 2017
124
190
VIJANA WAMEFIKA TAYARI GABON .​

-Timu ya Tanzania chini ya miaka kumi na Saba Serengeti boys imefika Tayari Gabon kwa mashindano ya AFCON (U17) Ambayo yataanza Jumapili Ijayo . Tanzania imefikia kwenye kituo chao cha Libreville ambapo zitachezewa mechi za kundi B. Msafara wa watu 30 Umefika na matumaini ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Makundi ya AFCON (u17)-2017
Kundi A. Kundi B.
-Gabon -Tanzania
-Ghana -Mali
-Cameroon -Angola
-Guinea -Niger

Ratiba ya Serengeti boys
May 15 vs Mali
May 18 vs Angola
May 21 vs Niger

mechi Saba za kirafiki hivi karibuni
Tanzania (U17) 3-0 Burundi (U17)
Tanzania (U17) 2-0 Burundi (17)
Tanzania (U17) 2-2 Ghana (U17)
Gabon (U17) 1-2 Tanzania (U17)
Gabon (U17) 1-2 Tanzania (U17)
Cameroon (U17) 0-1 Tanzania (U17)
Cameroon (U17) 1-0 Tanzania (U17)

JESHI KAMILI HILI HAPA
MAKIPA (3)
-Ramadhan Awm Kabwili,
-Samwel Edward Brazio
-Kelvin Deo Kayego

MABEKI (7)
-Kibwana Ally Shomary
-Nickson Clement Kibabage
-Israel Patrick Mwenda
-Dickson Nickson Job
-Ally Hussen Msengi
- Issa Mudy Makamba
- Enrick Vitalis Nkosi.

VIUNGO (9)
-Ally Hamis Ng'anzi
-Mohamed Rashid Chombo
-Shabaan Zubery Ada
- Mathias Juan Juan
-Marco Gerald Gerald
-Nashon Kelvin Naftali
-Cyprian Cybenedicto Mtesigwa
-Assad Juma Ally
-Bakari Said Mussa

WASHAMBULIAJI (4)
-Muhsin Malima Makame
-Oscar Yohana Mkomola
-Ibrahim Abdallah Ali
-Abdul Hamis Suleiman

BECHI LA UFUNDI
-Bakari Shime
(kocha mkuu)
-Oscar Mirambo
(kocha msaidizi)
-Muharami Mohamed
(kocha wa makipa)
-Kim Poulsen
(Mashauri wa ufundi)
-Edward Evans
(Mtunza Vifaa)
-Shecky Mngazija
(Daktari wa timu)

[HASHTAG]#GABONMPAKAKOMBELADUNIA[/HASHTAG]
-Tukutane Gabon

1249b3df6582cc2b65ef8351754b8a5d.jpg


======
Mashabiki wa soka wanaotaka kwenda Gabon kushuhudia mchezo mmoja wa Serengeti Boys hawana budi kujikamua Dola 1172 za Marekani sawa na zaidi ya Sh 2.6 milioni za Tanzania.serengeti Boys iko Gaboni na Mei 15 itaanza kampeni ya kusaka ubigwa wa mataifa ya Afrika kwa vijana kwa kuwavaa mabigwa watetezi Mali
akizungumza jijini Dar es salaam leo,mkurugenzi wa kampuni ya uwakala ya Luhesa Lukaya Sawe amesema kampuni yake kwa kushirikiana na TFF wameingia makubaliano ya kuratibu safari za mashabiki wa Tanzania wanaokwenda Gaboni kushuhudia fainali hizo
kwa mtu anayetaka kushuhudia mechi moja atalipa Dola 1172 ambazo zitajumuisha tiketi ya ndege kwenda na kurudi,hoteli,usafiri wa kwenda na kurudi uwanjani na kiingilio cha uwanjani Aliongeza kuwa shabiki atakaetaka kushuhudia mechi tatu za hatua ya makundi atalipa Dola 1770 (sawa na Sh 4m wakati mashabiki watakaokaa Gaboni wakati wote wa mashindano hayo watalipa Dola 2416 sawa na Sh 5.5 milioni
ca3277472db9b1cd422830ab87de1757.jpg

========
MICHUANO ya kugombea Ubingwa wa Afrika kwa Vijana chini ya Miaka 17, TOTAL U-17 AFCON GABON 2017, iliyoanza Jana kwa Mechi za Kundi A huko Nchini Gabon, Leo imeendelea kwa Mechi ya Kundi B kati ya Tanzania, maarufu kama Serengeti Boys, kutoka Sare 0-0 na Mali ambao ndio Mabingwa Watetezi.

Mechi hii ilichezwa Stade de L’Amitle, Mjini Libreville huko Gabon.

Hapo Jana, Wenyeji Gabon walianza vibaya kwa kutandikwa 5-1 na Guinea na kisha Ghana kuibonda Cameroun 4-1 zote zikiwa Mechi za Kundi A.

Baadae Leo, Mechi ya Pili ya Kundi A kati ya Angola v Niger itachezwa.

Mashindano haya yataendelea tena Jumatano kwa Mechi za Kundi A na Serengeti Boys kushuka tena dimbani Alhamisi kuivaa Angola ndani ya Stade de L’Amitle, Mjini Libreville huko Gabon.

Washindi Wawili wa kila Kundi watatinga Nusu Fainali na Timu hizo 4 zitakazocheza Nusu Fainali ndizo hizo hizo zitafuzu kucheza Fainali za FIFA za Kombe la Dunia kwa Vijana U-17 huko Nchini India Mwezi Oktoba.

Mechi ya 18/5/2017 Serengeti Boys vs Angola

Serengeti Boys imeifunga Angola goli 2-1

MATOKEO: Serengeti Boys 2-1 Angola (Full-Time)

Serengeti Boys imeandika ushindi wa kwanza wa michuano ya Afcon chini na taratibu ni dalili za kuingia hatua ya nusu fainali ambayo ni tiketi ya kucheza Kombe la Dunia.

Serengeti imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Angola na kupata pointi nne.

Mechi ya kwanza, Serengeti ilianza kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Mali ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Katika mchezo wa leo, Serengeti Boys ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 6 tu kupitia kwa Kelvin Naftali aliyeunganisha krosi safi ya Yohana Mkomola.

Angola awali ilijitutumua na kusawazisha katika dakika ya 18 kupitia kwa Pedro Augustino lakini Serengeti wakakomaa nao na kufunga bao la pili katika dakika ya 69 kwa bao la Abdul Selemani.


------------------------
Winga teleza wa Serengeti Boys, Abdul Suleiman aliyeibuka mchezaji bora wa mechi ya Serengeti Boys na Angola hapo jana, alichukuliwa na maafisa wa CAF na kufanyiwa vipimo vya dawa za kusisimua misuli.Hali hiyo ilisababisha ashindwe kwenda kupokea tuzo yake ya mchezaji bora hivyo akawakilishwa na mlinzi, Dickson Job. CAF hawakuamini walichokiona kwa Abdul ambaye alihaha uwanja mzima!Hata hivyo baada ya vipimo ilibainika hakuwa katumia dawa hizo bali ni uwezo binafsi wa mchezaji uwanjani. [HASHTAG]#GabonMpakaKombelaDunia[/HASHTAG]<br />.
736f15c77f8b30525f77953ae51400ad.jpg
e00a010daf35538bfac7b76e4c36fdeb.jpg

================
Serengeti Boys imewasili salama jijini Port Gentil, Gabon tayari kwa mchezo wa mwisho wa Kundi B dhidi ya Niger utakaochezwa Jumapili hii.
63278756a6786e308ebb7d84dd4df495.jpg
7e8cf936edce09932391c95244a0c87e.jpg
ed6191939889bc3f8a9a9d19089fc9b1.jpg
 
Tuko nyuma yenu nyie ndo mnaotuvuta. Kafanyeni kweli Gabon ili dunia ijue tupo.
 
Kila la kheri wachezaji wa timu ya chini ya umri wa miaka 17. Together we can. Tanzania taifa moja. Uzalendo kwanza
 
Nashauri hiyo timu iendelezwe ije kuwa timu rasimi ya taifa
Sio tunaungaunga mateja wa simba na yanga mwisho wa siku wanatuletea aibu na loss juu
 
Kuiona Serengeti Gabon bei poa

Mashabiki wa soka wanaotaka kwenda Gabon kushuhudia mchezo mmoja wa Serengeti Boys hawana budi kujikamua Dola 1172 za Marekani sawa na zaidi ya Sh 2.6 milioni za Tanzania.
serengeti Boys iko Gaboni na Mei 15 itaanza kampeni ya kusaka ubigwa wa mataifa ya Afrika kwa vijana kwa kuwavaa mabigwa watetezi Mali

akizungumza jijini Dar es salaam leo,mkurugenzi wa kampuni ya uwakala ya Luhesa Lukaya Sawe amesema kampuni yake kwa kushirikiana na TFF wameingia makubaliano ya kuratibu safari za mashabiki wa Tanzania wanaokwenda Gaboni kushuhudia fainali hizo
kwa mtu anayetaka kushuhudia mechi moja atalipa Dola 1172 ambazo zitajumuisha tiketi ya ndege kwenda na kurudi,hoteli,usafiri wa kwenda na kurudi uwanjani na kiinhilio cha uwanjani

Aliongeza kuwa shabiki atakaetaka kushuhudia mechi tatu za hatua ya makundi atalipa Dola 1770 (sawa na Sh 4m wakati mashabiki watakaokaa Gaboni wakati wote wa mashindano hayo watalipa Dola 2416 sawa na Sh 5.5 milioni
16865aaa7f6c26cd8671d09df075841c.jpg
 
Msisahau mambo ya fitina nje ya Uwanja, kuweni makini Kwny hilo, nidhamu na saikolojia
 
WACHEZAJI 21 WA SERENGETI BOYS WALIOPITISHWA NA CAF

MAKIPA (3)
-Ramadhan Awm Kabwili,
-Samwel Edward Brazio
-Kelvin Deo Kayego

MABEKI (7)
-Kibwana Ally Shomary
-Nickson Clement Kibabage
-Israel Patrick Mwenda
-Dickson Nickson Job
-Ally Hussen Msengi
- Issa Abdi Makamba
- Enrick Vitalis Nkosi.

VIUNGO (7)
-Ally Hamis Ng'anzi
-Mohamed Abdallah Rashid
-Shabaan Zubery Ada
-Nashon Kelvin Naftali
-Cyprian Benedict Mtesigwa
-Assad Juma Ally
-Bakari Said Mussa

WASHAMBULIAJI (4)
-Muhsin Malima Makame
-Yohana Oscar Mkomola
-Ibrahim Abdallah Ali
-Abdul Hamis Suleiman

5a928379a2d97f6a81887ce37b5abd40.jpg
 
Back
Top Bottom