Hapo ndo nasema hawa wapumbavu na wachumia tumbo wanaohangaika usiku kucha kuhakikisha hatukai na amani kwa tamaa zao za madaraka bora wauwawe wao kabla hawajaleta maafa makubwa kama haya.
Kikishasanuka hata mkulima hutomuona shambani, sokoni hutokuta misosi na matokeo yake unakuta raia kibao wanakufa na njaa. Bongo tuna umasikini wa vipato lakini sio misosi. Buku unakula wakati kuna nchi nyingine huwezi pata hata robo kilo ya unga kwa hilo buku.
Kila siku nasema wengi mnaoyabeza maisha ya bongo hamjapata fursa hata za kutembea kwa majirani zetu mf.Drc Congo,Somalia au Sudan kusini.. pote nimefika lakini maisha ya wenzetu yanasikitisha sana. Na kama umepitapita huko huwezi rudi bongo na akili ileile kama ulivyoenda.
Kuna kitu kitakufungua akili na kuona umuhimu wa nchi kukaa na amani. Hata kama tunataka mabadiliko zipo njia za kistaarabu za kuwashawishi wananchi na kujenga hoja ukaeleweka mwishowe ukapewa nafasi. Hapo ndo credit zangu zinaendaga kwa viongozi wanaoamini kwenye nguvu ya hoja na ushawishi kama Zitto Kabwe kuwa ndio wanatufaa kuwa viongozi wetu kuliko hawa wanaoamini kwenye siasa za ubabe, nguvu na, maandamano kwa kushindana na vyombo vya dola dizaini ya akina Lema.
Jamani ni hatari na tujihadhali sana na watu wa namna hii waliokosa uzalendo na wasiokuwa na huruma na damu za watu....