ACT Wazalendo walaani kitendo cha Serikali kusitisha Michezo mashuleni

karama kaila

Senior Member
Jan 30, 2015
122
60
TAARIFA KWA UMMA

NGOME YA VIJANA, ACT WAZALENDO KULAANI HATUA YA SERIKALI KUSITISHA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA.

SIKU ya tarehe 13/06/2016 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene aliutangazia Ummma wa watanzania kuwa serikali imeamua kusitisha mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za msingi na Sekondari Nchini (Umitashumta na Umisseta) ambayo ilipangwa kuanza kitaifa jijini Mwanza kuanzia Juni 13 na kumalizikia Julai 5 Mwaka huu.

Waziri Simbachawene ameeleza kuwa sababu ya kufanya hivyo ni Kupisha zoezi la Kumalizia Ukamilishaji wa madawati ili kutimiza agizo la Rais la kuondoa Upungufu wa Madawati kwa shule za msingi na sekondari Nchini.

Kwamba fedha ambazo zingetumika katika michezo hiyo zielekezwe kwenye madawati na wadau ambao wangesimamia michezo yote kwa shule ya msingi na sekondari wajikike katika kukamilisha upatikanaji wa madawati hayo

Sisi vijana wa Ngome ya ACT wazalendo na Taifa kwa ujumla tunajua Kuwa Wanafunzi si Mafundi wa Madawati, Kazi hiyo ni ya Mafundi Mchundo na Kampuni mbalimbali zilizopewa zabuni ya Utengenezaji wa Madawati husika, hivyo tunauona Umamuzi huu wa kusitisha Mashindano haya Kuwa ni Ukiukwaji wa Haki za Mtoto kucheza na Unaondoa Msingi Muhimu wa Taaluma na Michezo Kwa Vijana wa Taifa hili.

Pia ni muendelezo wa mawaziri wa serikali ya awamu ya tano kufanya kazi kwa mihemko pasipo kutafakari athari ya kile wanachotaka kukifanya, Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Tunapinga Vikali na Kulaani Uamuzi huu wa Serikali wa Kukandamiza na Kupora Haki ya Msingi kwa Watoto wa Kitanzania ya Kucheza Bila Sababu za Msingi.

Kazi ya Usimamizi wa Mashindano hayo ni Kazi ya Maafisa Utamaduni Na Michezo wa Wilaya Na Mikoa, hivyo hao wanaoitwa Na Waziri Kuwa ni "Wadau Muhimu katika uamuzi huo wa Utengenezaji wa Madawati si Wasimamizi wa Mashindano Haya ya Vijana.

Vijana wa ACT Wazalendo tunajua Kuwa Bajeti ya Fedha za Kugharamia Michezo hii ilipitishwa na bunge kwenye bajeti ya Mwaka 2015/16, tunaona Utaratibu wa Kupeleka Kasma Husika kwenye Matumizi Mengine si tu umewanyima Haki ya Kucheza Vijana wa Taifa hili Lakini pia ni Ukiukwaji wa taratibu za matumizi ya Serikali.

Mbali na ukiukwaji wa utaratibu katika bajeti iliyopitishwa na bunge pia uamuzi huu wa serikali unazidi kuichimbia kaburi vipaji vya vijana wenzetu ambao wangeweza kupatikana katika michezo hiyo na kuiletea sifa nchi katika siku za usoni

Pia katika uamuzi huu tunaouita kuwa usio na tija kwa Taifa ni wazi serikali imeridhia kukiuka mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto (UN Convention On Rights of The Child). Mkataba huu chini ya ibara ya 31 unahimiza haki ya Kila mtoto kucheza na kupata muda wa ukpumzika (Right to play and rest).

Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2009 lilitunga na Kupitisha Sheria ya Mtoto ambayo Kifungu Cha 8(1) (g) imesisitiza Juu ya Haki za Mtoto kucheza na kupumzika. Usitishaji wa Mashindano haya si tu unavunja Sheria za nchi yetu na unakiuka Kabisa mkataba wa Umoja wa Mataifa, Hatua Ambayo itaipa Sifa Mbaya nchi yetu Kimataifa.

Ibara ya 3 ya Mkataba huu inataka Maamuzi yote Juu ya hatima ya Watoto na Vijana yafanyike Kwa kuangalia athari zake Kwao, Maamuzi haya ya Serikali hayajazingatia athari husika.

Vijana wa ACT Wazalendo tunaamini Kuwa Serikali ya CCM haijui na haithamini Umuhimu wa Michezo kwa Watoto na faida ya Mashindano ya Umitashumta na Umisseta Taifa.

maamuzi haya Mabaya ya Serikali ni ya kuwakatisha tamaa wadau wa Michezo Na Sanaa Nchini, Na yanabinya fursa ya Uvumbuzi wa Vipaji vya Watoto na Vijana. Ni muhimu Serikali ijue kuwa Michezo sio nyongeza, Michezo sio ziada, Michezo ni Haki ya Watoto kama zilivyo haki nyingine.

Vijana wa ACT Wazalendo tunaitaka Serikali ya Rais Magufuli, Kusitisha Mbio za Mwenge wa Uhuru ili Fedha zinazotumika kuuzungusha Nchi nzima zitumike kutengenezea madawati. Na kuwaachia Jukumu la Usimamizi wa Mashindano Haya Maafisa Utamaduni Na Michezo Kama inavyotakikana na hao "Wadau Muhimu" wa Waziri Simbachawene Waendelee Na zoezi la Utengenezaji wa Madawati.

Mwisho tunatoa Wito kwa Taasisi zote zinazopigania na kutetea Haki za Watoto kusimama pamoja katika kuhakikisha Watoto wa Kitanzania waliopo mashuleni wanaendelea kupata haki yao ya kucheza na kuitaka Serikali iwajibike katika ipasavyo kuhakikisha inatimiza wajibu wake kwa Watoto.

Imetolewa na
Likapo B. Likapo
Mratibu Taifa Ngome ya Vijana
ACT-Wazalendo
17/06/2016
 
Na mawazo mbadala mmewapa.....pesa za mbio za mwenge zikatumike kutengeza madawati......kina samata waibuliwe
 
Aiseee , Mimi pia napenda michezo na ningependa michezo ipewe kipaumbele! Lakini najiuliza ni haki mtoto kukaa chini darasani ? na nani kasababisha? Je ,ni kweli hiyo sababu ni ya usimamizi au ukosefu wa fedha? Maswali mengi majibu hakuna. Anyway tuichie serikali ,maana hata hao wanaochaguliwa kwenda baadhi sio wenye vipaji halisi ni full figisu .
 
Tuiendelee kuikumbusha Serikali, inajisahau sana

Nafikiri kuna shida kubwa zaidi ya serikali kujisahau. BUNGE letu sasa haliisimamii serikali, bali SERIKALI inaliongoza Bunge. Inakuwaje reallocation ya fedha za umma ambazo ziliidhinishwa na Bunge baada ya kujadiliwa leo hii zikabadilishiwe matumizi na wabunge wasihoji?
 
Aiseee , Mimi pia napenda michezo na ningependa michezo ipewe kipaumbele! Lakini najiuliza ni haki mtoto kukaa chini darasani ? na nani kasababisha? Je ,ni kweli hiyo sababu ni ya usimamizi au ukosefu wa fedha? Maswali mengi majibu hakuna. Anyway tuichie serikali ,maana hata hao wanaochaguliwa kwenda baadhi sio wenye vipaji halisi ni full figisu .

Si haki ya mtoto kukaa chini, lakini si haki ya serikali unayosema tuiachie kubadilisha matumizi ya fedha ambazo ziliidhinishwa na bunge. Michezo sio 'mizaha' kama inavyotafsirika hapa. Michezo ni kama ufundi mwingine. Wakati itazungumzika kama inamaanisha kidari na mdako tukumbuke kuwa kuna wengine ambao future yao iko viwanjani.

Yale madawati 600 aliyotoa Diamond yametoka kwenye sanaa na sio kwenye siasa. Kama juzi juzi walimpeleka Mbwana Samata bungeni na kujisifia as if wao ndio walimnunulia viatu alivyochezea mchangani, basi UMISETA na UMISHUMTA ndio darasa la kutengeneza kina Samata wengine.

Madawati hayajaanza kukosekana leo.
 
viongozi wa ccm sijui wanafikiri kwa kutumia nini,ndio maana nilisema kwamaba ili tupate maendeleo na kuwa Tanzania ya viwanda ni lazima kwanza ccm itoke madarakani, hivi kufuta hiyo michezo kunasaidia nini madawati kwa nini wasifute mbio za mwenge?
 
Ule utaratibu mzuri uliokuwa ukitumika zamani wa shule zilizopo ndani ya Tarafa kucheza kati ya shule moja na shule nyingine ili kutoa fursa ya kupata vipaji ktk kila shule ili wakutane katika UMISETA/UMISHUMTA wilayani kupata timu ya wilaya ambayo inakwenda kuwakilisha mkoa haupo.

Badala yake kila shule inatoa mwanafunzi mmoja mmoja au wawili bila ya kucheza mechi kuonekana vile vipaji vyao wanapelekwa mchujo katika wilaya, bajeti ni ndogo kwenye michezo na utaratibu unaotumika unaua vipaji kwa watoto wetu kwani hawapati hamasa ya michezo.

Viwanja vinavyotumika kwa michezo ya UMISETA/UMISHUMTA wilayani ni vibovu, magoli ya miti, havina nafasi ya kukimbia riadha, michezo mingine kama volleyball, basketball na kurusha tufe haichezwi mpk wakifika mkoani ndio wanaikuta, nyavu za goalpost ni kamba za katani zimefungwa fungwa.

Michezo kwa wanafunzi ni mazoezi, mwanafunzi akiwa na afya nzuri ufaulu wake unakuwa mzuri, michezo ni ajira. Kuna wanafunzi ufaulu wao sio mzuri darasani lakini wana vipaji katika michezo eg. Samatta

Serikali isipuuzie michezo bali iweke mikakati mizuri kwa wanafunzi kulinda vipaji kuanzia shule za msingi, secondary mpk kwenye academy..pia wasiishie kwa msingi na sekondari tu bali wajenge hadi vyuo vya kuendeleza michezo nchini
 
Wanajf, kwanza niwakumbushe kuwa bunge halikuwahi kukutana na kupitisha fedha za elimu bure ambapo ndani yake ndio kuna mchanganuo wa fedha za michezo, ukarabati na matumizi ya ofisi. Kusitishwa kwa fedha hizi hakuhitaji bunge pia hata kama zilitumika kuandaa timu hadi ngazi ya mkoa. Sasa jiulize fedha nyingi ni zipi kati ya kupeleka timu kitaifa au zile zilizotumika kuandaa timu tangu ngazi ya shule hadi mkoa? Hizi zilizobaki zitatengeneza madawati mangapi?
Kwa haraka tu ni kuwa mpango mzima wa kupata madawati kwa muda waliojipangia umefeli kwani wenye watoto au wadau wa elimu hawakupewa nafasi ya kujadili na wameburuzwa. Na hata waziri anazidi kuwaburuza wadau kwani hatujui hili fungu linachotwaga wizara gani.
 
Sisi kwenye hili lichama letu la mashetani(ccm) tunathamini zaidi mbio za mwenge kuliko haki za watoto wenu vi-la-za ndio maana hata michango ya mwenge tunaifanya ni ya lazima kisheria lakini haki za watoto wetu tunamuachia hata kichaa mmoja tu azisigine na mnachotakiwa kufanya ni kumshangilia tu mfalme kama sivyo kamanda Ziro anatuma maroboti yake kuzunguka nyumba zenu!
 
Washauri wa serikali hii utadhani wanaota mchana na usiku. Huku ndio kubana matumizi? Ingeweka mikakati kupunguza gharama basi mashindano ya michezo yafanyike within province lakini kusitisha michezo mashuleni huu ni ubuyuyu sasa. Enzi za Nyerere michezo mashuleni ilifanikiwa sana kwa nini tushindwe sasa? Futeni vikao vikao vyenu visivyo na tija kwa taifa elekezeni akili zenu kwenye Elimu Kilimo Uvuvi Viwanda Biashara nchi itasimama
 
TAARIFA KWA UMMA

NGOME YA VIJANA, ACT WAZALENDO KULAANI HATUA YA SERIKALI KUSITISHA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA.

SIKU ya tarehe 13/06/2016 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene aliutangazia Ummma wa watanzania kuwa serikali imeamua kusitisha mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za msingi na Sekondari Nchini (Umitashumta na Umisseta) ambayo ilipangwa kuanza kitaifa jijini Mwanza kuanzia Juni 13 na kumalizikia Julai 5 Mwaka huu.

Waziri Simbachawene ameeleza kuwa sababu ya kufanya hivyo ni Kupisha zoezi la Kumalizia Ukamilishaji wa madawati ili kutimiza agizo la Rais la kuondoa Upungufu wa Madawati kwa shule za msingi na sekondari Nchini.

Kwamba fedha ambazo zingetumika katika michezo hiyo zielekezwe kwenye madawati na wadau ambao wangesimamia michezo yote kwa shule ya msingi na sekondari wajikike katika kukamilisha upatikanaji wa madawati hayo

Sisi vijana wa Ngome ya ACT wazalendo na Taifa kwa ujumla tunajua Kuwa Wanafunzi si Mafundi wa Madawati, Kazi hiyo ni ya Mafundi Mchundo na Kampuni mbalimbali zilizopewa zabuni ya Utengenezaji wa Madawati husika, hivyo tunauona Umamuzi huu wa kusitisha Mashindano haya Kuwa ni Ukiukwaji wa Haki za Mtoto kucheza na Unaondoa Msingi Muhimu wa Taaluma na Michezo Kwa Vijana wa Taifa hili.

Pia ni muendelezo wa mawaziri wa serikali ya awamu ya tano kufanya kazi kwa mihemko pasipo kutafakari athari ya kile wanachotaka kukifanya, Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Tunapinga Vikali na Kulaani Uamuzi huu wa Serikali wa Kukandamiza na Kupora Haki ya Msingi kwa Watoto wa Kitanzania ya Kucheza Bila Sababu za Msingi.

Kazi ya Usimamizi wa Mashindano hayo ni Kazi ya Maafisa Utamaduni Na Michezo wa Wilaya Na Mikoa, hivyo hao wanaoitwa Na Waziri Kuwa ni "Wadau Muhimu katika uamuzi huo wa Utengenezaji wa Madawati si Wasimamizi wa Mashindano Haya ya Vijana.

Vijana wa ACT Wazalendo tunajua Kuwa Bajeti ya Fedha za Kugharamia Michezo hii ilipitishwa na bunge kwenye bajeti ya Mwaka 2015/16, tunaona Utaratibu wa Kupeleka Kasma Husika kwenye Matumizi Mengine si tu umewanyima Haki ya Kucheza Vijana wa Taifa hili Lakini pia ni Ukiukwaji wa taratibu za matumizi ya Serikali.

Mbali na ukiukwaji wa utaratibu katika bajeti iliyopitishwa na bunge pia uamuzi huu wa serikali unazidi kuichimbia kaburi vipaji vya vijana wenzetu ambao wangeweza kupatikana katika michezo hiyo na kuiletea sifa nchi katika siku za usoni

Pia katika uamuzi huu tunaouita kuwa usio na tija kwa Taifa ni wazi serikali imeridhia kukiuka mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto (UN Convention On Rights of The Child). Mkataba huu chini ya ibara ya 31 unahimiza haki ya Kila mtoto kucheza na kupata muda wa ukpumzika (Right to play and rest).

Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2009 lilitunga na Kupitisha Sheria ya Mtoto ambayo Kifungu Cha 8(1) (g) imesisitiza Juu ya Haki za Mtoto kucheza na kupumzika. Usitishaji wa Mashindano haya si tu unavunja Sheria za nchi yetu na unakiuka Kabisa mkataba wa Umoja wa Mataifa, Hatua Ambayo itaipa Sifa Mbaya nchi yetu Kimataifa.

Ibara ya 3 ya Mkataba huu inataka Maamuzi yote Juu ya hatima ya Watoto na Vijana yafanyike Kwa kuangalia athari zake Kwao, Maamuzi haya ya Serikali hayajazingatia athari husika.

Vijana wa ACT Wazalendo tunaamini Kuwa Serikali ya CCM haijui na haithamini Umuhimu wa Michezo kwa Watoto na faida ya Mashindano ya Umitashumta na Umisseta Taifa.

maamuzi haya Mabaya ya Serikali ni ya kuwakatisha tamaa wadau wa Michezo Na Sanaa Nchini, Na yanabinya fursa ya Uvumbuzi wa Vipaji vya Watoto na Vijana. Ni muhimu Serikali ijue kuwa Michezo sio nyongeza, Michezo sio ziada, Michezo ni Haki ya Watoto kama zilivyo haki nyingine.

Vijana wa ACT Wazalendo tunaitaka Serikali ya Rais Magufuli, Kusitisha Mbio za Mwenge wa Uhuru ili Fedha zinazotumika kuuzungusha Nchi nzima zitumike kutengenezea madawati. Na kuwaachia Jukumu la Usimamizi wa Mashindano Haya Maafisa Utamaduni Na Michezo Kama inavyotakikana na hao "Wadau Muhimu" wa Waziri Simbachawene Waendelee Na zoezi la Utengenezaji wa Madawati.

Mwisho tunatoa Wito kwa Taasisi zote zinazopigania na kutetea Haki za Watoto kusimama pamoja katika kuhakikisha Watoto wa Kitanzania waliopo mashuleni wanaendelea kupata haki yao ya kucheza na kuitaka Serikali iwajibike katika ipasavyo kuhakikisha inatimiza wajibu wake kwa Watoto.

Imetolewa na
Likapo B. Likapo
Mratibu Taifa Ngome ya Vijana
ACT-Wazalendo
17/06/2016
Du! Kweli vijana hawa ni wa ajabu sana! Wako radhi watoto waendelee kuketi mchangani ama sakafuni lakini fedha zitumike kuwaburudisha kucheza! Kuh Mwenge was Uhuru inadhihirisha jinsi gani vijana wenye mawazo ya aina hii hhawaienzi wala kuithamini historia ya nchi yao! Aibu sana!
 
Back
Top Bottom