ACT Wazalendo kufanya mikutano yenye jina la 'Linda Demokrasia'

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
CHAMA CHA ACT WAZALENDO

TAARIFA KWA UMMA

Leo Juni 3/2016 Chama cha ACT Wazalendo Kimeelezea msimamo wake juu ya uamuzi uliofanywa na Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuwasimamisha wabunge saba wa upinzani akiwemo Mbunge wa ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe.

Uamuzi huu wa Kamati ya Maadili ambayo sehemu kubwa ya wajumbe wake ni wabunge wa Chama cha Mapinduzi(CCM) unafuatia msimamo wa wabunge wa upinzani wakiongozwa na Mbunge wa Chama chetu kupigania maslahi ya wananchi kupata habari za bunge.

ACT Wazalendo inaamini Wabunge hawa wametolewa kafara kwa kupinga vikali uamuzi wa Serikali kuzuia matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja.

Chama kimeandaa mapokezi haya yaliyopewa jina maalum la “Opereshen” Linda Demokrasia, lengo likiwa ni kuwapa nafasi mashujaa waliofukuzwa bungeni kwa ajili ya kusimamia maslahi ya umma, kuelezea kilichotokea na kinachoendelea bungeni ambacho watawala hawataki kijulikane.

Pia katika mkutano wa hadhara Kiongozi wa Chama ndugu Zitto Kabwe atafafanua kwa kina muktadha wa siasa za sasa na hatari ya kuua vita dhidi ya ufisadi kutokana na namna demokrasia inavyofifishwa

Kwa kutambua umuhimu wa utetezi wa maslahi ya wananchi na kuisimamia serikali kupitia Bunge Chama chetu baada ya mkutano wa Dar esSalaam utakaofanyika Jumapili ya Juni 5 mwaka huu katika viwanja vya Mbagala Zakiem, pia Chama kitafanya mikutano mingine mikubwa ya hadhara katika mikoa ya Mwanza ( 11 Juni, 2016), Kigoma (12 Juni, 2016), Mbeya (18 Juni, 2016) na Morogoro (19 Juni, 2016).

Chama imeviandikia barua vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi kuviomba kushiriki kwenye mapokezi hayo.Tunasubiri majibu ya vyama tulivyowaalika kwa kuwaandikia barua kwa kuwa mpaka sasa hawajatujibu rasmi kama watashiriki ama la zaidi ya kutufahamisha kuwa wamepokea barua zetu

ACT-Wazalendo,inaamini “Operesheni Linda Demokrasia” ni muhimu ikapiganwa na vyama vyote pasipo kujali itakadi ya vyama kwa kuwa hoja hiyo ya kutaka Bunge lioneshwe moja kwa moja ilipoibuliwa na Mbunge Ndugu Zitto Kabwe kuhoji hatua ya serikali kubana uwazi Bungeni,wabunge wote wa upinzani walisimama na kuiunga mkono hoja na kuitetea

Ndugu Ado Shaibu Ado

Katibu, Itikadi Uenezi na Mawasiliano ya Umma,

ACT Wazalendo
 
Kwanini msingesema vyama vya upinzani vinawaalika wananchi wote kushiriki mkutano mkubwa badara yake ajenda nzima mmeibeba nyinyi ACT? UKAWA na nyie shambulieni mikoa mingine mfano Tundu Lissu Singida.. Sugu Mbeya.. Bulaya.. Bunda.. Lema Arusha nk.
 
CHAMA CHA ACT WAZALENDO

TAARIFA KWA UMMA

Leo Juni 3/2016 Chama cha ACT Wazalendo Kimeelezea msimamo wake juu ya uamuzi uliofanywa na Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuwasimamisha wabunge saba wa upinzani akiwemo Mbunge wa ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe.

Uamuzi huu wa Kamati ya Maadili ambayo sehemu kubwa ya wajumbe wake ni wabunge wa Chama cha Mapinduzi(CCM) unafuatia msimamo wa wabunge wa upinzani wakiongozwa na Mbunge wa Chama chetu kupigania maslahi ya wananchi kupata habari za bunge.

ACT Wazalendo inaamini Wabunge hawa wametolewa kafara kwa kupinga vikali uamuzi wa Serikali kuzuia matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja.

Chama kimeandaa mapokezi haya yaliyopewa jina maalum la “Opereshen” Linda Demokrasia, lengo likiwa ni kuwapa nafasi mashujaa waliofukuzwa bungeni kwa ajili ya kusimamia maslahi ya umma, kuelezea kilichotokea na kinachoendelea bungeni ambacho watawala hawataki kijulikane.

Pia katika mkutano wa hadhara Kiongozi wa Chama ndugu Zitto Kabwe atafafanua kwa kina muktadha wa siasa za sasa na hatari ya kuua vita dhidi ya ufisadi kutokana na namna demokrasia inavyofifishwa

Kwa kutambua umuhimu wa utetezi wa maslahi ya wananchi na kuisimamia serikali kupitia Bunge Chama chetu baada ya mkutano wa Dar esSalaam utakaofanyika Jumapili ya Juni 5 mwaka huu katika viwanja vya Mbagala Zakiem, pia Chama kitafanya mikutano mingine mikubwa ya hadhara katika mikoa ya Mwanza ( 11 Juni, 2016), Kigoma (12 Juni, 2016), Mbeya (18 Juni, 2016) na Morogoro (19 Juni, 2016).

Chama imeviandikia barua vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi kuviomba kushiriki kwenye mapokezi hayo.Tunasubiri majibu ya vyama tulivyowaalika kwa kuwaandikia barua kwa kuwa mpaka sasa hawajatujibu rasmi kama watashiriki ama la zaidi ya kutufahamisha kuwa wamepokea barua zetu

ACT-Wazalendo,inaamini “Operesheni Linda Demokrasia” ni muhimu ikapiganwa na vyama vyote pasipo kujali itakadi ya vyama kwa kuwa hoja hiyo ya kutaka Bunge lioneshwe moja kwa moja ilipoibuliwa na Mbunge Ndugu Zitto Kabwe kuhoji hatua ya serikali kubana uwazi Bungeni,wabunge wote wa upinzani walisimama na kuiunga mkono hoja na kuitetea

Ndugu Ado Shaibu Ado

Katibu, Itikadi Uenezi na Mawasiliano ya Umma,

ACT Wazalendo
Hawa wanasiasa wa Tanzania wajinga kweli, ati sasa wanaungana kupambana na serikali, wakati muafaka wa kuitoa serikali madarakani kila moja alikua na lake. Ndiyo maana CCM wanafanya wanavyotaka maana huu upinzani wetu ni bure kabisa. Hii habari ya ATC inanikumbusha mwaka 1995 katika uchaguzi NCCR walidhani wangeshinda uchaguzi sababu ya joto Mrema wakakataa kuungana na wenzao matokeo ya uchaguzi yalipotoka na kupigwa chini nikawaona wote wanaungana kwenda mahakamani kupinga matokeo wakati walijua NEC ikishamtangaza rais mahakama haina uwezo wa kutengua. Hivi watanzania lini tutabadilika kuwaonyesha ccm na wapinzani kuwa sisi siyo wajinga kama wanavyofikiria? Hapa ndani tumebaki kushabikia hata ujinga iwe wa CCM, wa Magufuli ama wa upinzani. Hawa jamaa wote wapiga deal na wanavyoona tunajigawa kwa misingi ya itikadi pande zote zinafurahi.
 
Tatizo la wanasiasa ni luwa na ego zinazopitiliza...

Unapoanza kubinafsisha hoja ni upuuzi...

Washirikiane lakini sio kwa mtindo huu!!
 
Hawa wanasiasa wa Tanzania wajinga kweli, ati sasa wanaungana kupambana na serikali, wakati muafaka wa kuitoa serikali madarakani kila moja alikua na lake. Ndiyo maana CCM wanafanya wanavyotaka maana huu upinzani wetu ni bure kabisa. Hii habari ya ATC inanikumbusha mwaka 1995 katika uchaguzi NCCR walidhani wangeshinda uchaguzi sababu ya joto Mrema wakakataa kuungana na wenzao matokeo ya uchaguzi yalipotoka na kupigwa chini nikawaona wote wanaungana kwenda mahakamani kupinga matokeo wakati walijua NEC ikishamtangaza rais mahakama haina uwezo wa kutengua. Hivi watanzania lini tutabadilika kuwaonyesha ccm na wapinzani kuwa sisi siyo wajinga kama wanavyofikiria? Hapa ndani tumebaki kushabikia hata ujinga iwe wa CCM, wa Magufuli ama wa upinzani. Hawa jamaa wote wapiga deal na wanavyoona tunajigawa kwa misingi ya itikadi pande zote zinafurahi.
Mkuu, hakuna mtanzania atakayeungana na LOWASSA kumpinga Magufuli, huyo atakuwa mjinga kupindukia. Hatuwezi kukubali kurudi shimoni wakati Magufuli kajitoa sadaka kututoa huko.
 
Kama ilivyotokea kwa NCCR-MAGEUZI, CUF na NLD, naliona anguko la ACT-WAZALENDO. Zitto akishavuliwa tu na nyavu za CHADEMA hakuna tena ACT.
 
Nyie tafuteni KICK huko majukwaani, Watanzania tuko na Magufuli wetu.
Mkuu mimi naungana na mambo mengi ambayo magufuli anayafanya na ninajua kuwa anayafanya kwa moyo moja lakini ninakwazika na kasi yake ya kukurupuka na kwenda kwenye vyombo vya habari sijaona kiongozi yeyote wa nchi anaekimbilia ktk media kama huyu wetu. hata kama anakwenda katika media kuna maamuzi mengine hatakiwi kuyatoa katia mikutana ya hadhara, hakuna mtu atakuona upo serious, jana kasema waliofeli wanakwenda udom na watoto wa viongozi leo kuna mtu hapa katuletea mada na kopi ya cheti cha mtoto wake hapo huoni kama na yeye ana makosa? Ninyi wapenzi wa Magufuli na wa Lowasa msipende kututukana tukitoa maoni yasiyoendana na mawazo yenu sababu sisi ni watanzania tunamuunga mkono kiongozi yeyote awe wa upinzani ama wa serikali pale tunapoona ameonyesha imani kwa nchi lakini mimi binafsi sipo tayari kushabikia vyama.
 
Mkuu mimi naungana na mambo mengi ambayo magufuli anayafanya na ninajua kuwa anayafanya kwa moyo moja lakini ninakwazika na kasi yake ya kukurupuka na kwenda kwenye vyombo vya habari sijaona kiongozi yeyote wa nchi anaekimbilia ktk media kama huyu wetu. hata kama anakwenda katika media kuna maamuzi mengine hatakiwi kuyatoa katia mikutana ya hadhara, hakuna mtu atakuona upo serious, jana kasema waliofeli wanakwenda udom na watoto wa viongozi leo kuna mtu hapa katuletea mada na kopi ya cheti cha mtoto wake hapo huoni kama na yeye ana makosa? Ninyi wapenzi wa Magufuli na wa Lowasa msipende kututukana tukitoa maoni yanaoendana na mawazo yenu sababu sisi ni watanzania tunamuunga mkono kiongozi yeyote awe wa upinzani ama wa serikali pale tunapoona ameonyesha imani kwa nchi lakini mimi binafsi sipo tayari kushabikia vyama.
Huko kukurupuka ndiko Watanzania tulikukosa muda mrefu ili mambo yaende. Subirini wasiyokurupuka miaka hiyo ya kufikirika.
 
Dah wewe unanikumbusha wale waliosema wako tayari kuchagua jiwe liwaongoze kuliko ccm hata kama aliyewekwa ni msafi. Sina la zaidi kwa mtaji huu tusubiri miujiza ya Mola.
 
Katibu wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO SHAIBU akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi ya kumpokea kiongozi yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE ambaye naye amekumbwa na timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo yatafanyika Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili

Story ambayo bado ipo maskioni mwa watanzania walio wengi ni mwenendo wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na mizengwe yake ambayo imesababisha wabunge saba wa vyama vya upinzani kusimamiswa kushiriki shughuli za bunge kwa vipindi Tofauti tofauti akiwemo mbunge kutoka ndani ya chama cha Act wazalendo Mh ZITTO ZUBERI KABWE na wabunge wa vyama vya UKAWA.

Sakata hilo limeendelea kuchukua Headline katika maeneo mbalimbali ambapo asubuhi hii chama cha ACT wazalendo kupitia kwa kiongozi wao ADO SHAIBU wamejitokeza mbele ya wanahabari kueleza msimamo wa chama chao kuhusu sakata hilo.

Akizungumza na wanahabari leo Katibu huyo wa itikadi mawasiliano na uenezi wa ACT ADO SHAIBU ameeleza kuwa chama hicho kimeandaa mapokezi ya kiongozi wao ambaye amekumbwa na adhabu hiyo mapokezi ambayo yanataraji kufanyika Jijini Dar es salaam na baadae kufwatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara ambao umepangwa kufanyika katika viwanja vya ZAKIEM mbagala lengo likiwa ni kuwapa nafasi wabunge hao kueleza ukweli wa yale yanayoendelea bungeni Dodoma.

Pamoja na mandalizi hayo chama hicho kimewaandikia barua makatibu wa vyama vya upinzani ambao nao wanapinga adhabu hiyo kutoka CHADEMA,CUF,na NCCR-MAGEUZI kuwaomba kuungana nao katika mapokezi hayo ambayo yamepewa jina la OPERATION LINDA DEMOCRASIA na bado hawajapata majibu yao lakini wanaamini wataungana nao katika Operation iyo ambayo itafwatiwa na mikoa mingine takribani minne.
 
Mkuu, hakuna mtanzania atakayeungana na LOWASSA kumpinga Magufuli, huyo atakuwa mjinga kupindukia. Hatuwezi kukubali kurudi shimoni wakati Magufuli kajitoa sadaka kututoa huko.
Kutuuzia sukari kilo elfu 6 na kutuzuia tusifanye kazi usiku na kutupangia muda wa kuuza vileo uanze saa 9 na kufungwa saa nne?
 
Back
Top Bottom