ACT Wazalendo: Kauli ya Rais Magufuli ni vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama vingi nchini

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,211
2,328
Kauli ya Rais ya Kuzuia Vyama vya Siasa Kufanya Shughuli za Siasa kwa Miaka Mitano ni Tangazo la Vita dhidi ya Demokrasia na Mfumo wa Vyama vingi Nchini

Tumepokea kwa MSHTUKO na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa Kampeni na kupitia bungeni. Kimsingi kauli ya Rais ni kauli yenye nia ya kuvunja Sheria ya Vyama vya siasa inayolinda uwepo wa mfumo wa vyama vingi na kuhimiza vya vya siasa kufanya shughuli za siasa katika msimu wote ili kuthibitisha uhai wao.

Tunaichukulia kauli ya Rais kama tangazo la vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama vingi nchini. Chama chetu kitaitisha vikao vya dharura kujadili hali ya siasa nchini na namna ya kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya demokrasia nchini mwetu.

Tunatoa wito kwa vyama vyote vya siasa vinavyoamini katika misingi ya demokrasia nchini kukutana haraka na kujadili namna ya kuunganisha nguvu pamoja katika kupigana vita mpya ya kulinda demokrasia nchini mwetu.

Aidha, tunatoa wito kwa wananchi wote na taasisi za kiraia kusimama imara katika kulinda demokrasia. Tunasisitiza kuwa ushahidi wa kisayansi duniani kote unaonyesha kuwa huwezi kuua demokrasia bila kuua juhudi za maendeleo. Tusiruhusu mtu yeyote mwenye mamlaka kuua demokrasia nchini mwetu.Hatua zozote za kuua demokrasia ni kuua Umoja, Amani na Mshikamano wa wananchi na Taifa, ambayo ndiyo misingi ya maendeleo ya nchi yetu kijamii, kisiasa na kiuchumi. Tunatoa wito kwa wananchi wote kushikamana na kusimama imara katika kipindi hiki kigumu ili kulinda demokrasia.

Zitto Kabwe, MB
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Alhamisi, 23 Juni 2016.
 
Namuunga mkono Rais Magufuli, huu ni wakati wa kufanya harakati za kimaendeleo, na sio harakati za kisiasa.

Wakati mwingine tuangalie nchi zilizoendelea zinafanyaje mambo yao.

Siasa zimechangia sana kutugawa, kuturudisha nyuma, kutupotezea muda, kutujengea chuki na kutuacha masikini tusiofanya kazi kwa kutegemea matarajio hewa ya kisiasa.

Kauli njema ya Mh Rais haikubagua wala kupendelea chama. Ni vema watanzania tukumbuke kuwa kuna watu wananufaika na hizi dili za kisiasa, na lazima walalamike.

Rais amesema, uchaguzi umekwisha, na tulioshinda ni watanzania.

Ni wakati sasa wa kuwa watanzania, ni wakati wa kuungana katika mambo ya msingi, na kujiletea maendeleo.
 
Kauli ya Rais ya Kuzuia Vyama vya Siasa Kufanya Shughuli za Siasa kwa Miaka Mitano ni Tangazo la Vita dhidi ya Demokrasia na Mfumo wa Vyama vingi Nchini

Tumepokea kwa MSHTUKO na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa Kampeni na kupitia bungeni. Kimsingi kauli ya Rais ni kauli yenye nia ya kuvunja Sheria ya Vyama vya siasa inayolinda uwepo wa mfumo wa vyama vingi na kuhimiza vya vya siasa kufanya shughuli za siasa katika msimu wote ili kuthibitisha uhai wao.

Tunaichukulia kauli ya Rais kama tangazo la vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama vingi nchini. Chama chetu kitaitisha vikao vya dharura kujadili hali ya siasa nchini na namna ya kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya demokrasia nchini mwetu.

Tunatoa wito kwa vyama vyote vya siasa vinavyoamini katika misingi ya demokrasia nchini kukutana haraka na kujadili namna ya kuunganisha nguvu pamoja katika kupigana vita mpya ya kulinda demokrasia nchini mwetu.

Aidha, tunatoa wito kwa wananchi wote na taasisi za kiraia kusimama imara katika kulinda demokrasia. Tunasisitiza kuwa ushahidi wa kisayansi duniani kote unaonyesha kuwa huwezi kuua demokrasia bila kuua juhudi za maendeleo. Tusiruhusu mtu yeyote mwenye mamlaka kuua demokrasia nchini mwetu.Hatua zozote za kuua demokrasia ni kuua Umoja, Amani na Mshikamano wa wananchi na Taifa, ambayo ndiyo misingi ya maendeleo ya nchi yetu kijamii, kisiasa na kiuchumi. Tunatoa wito kwa wananchi wote kushikamana na kusimama imara katika kipindi hiki kigumu ili kulinda demokrasia.

Zitto Kabwe, MB
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Alhamisi, 23 Juni 2016.

VYAMA VYA SIASA VIKUTANE HARAKA TENA MAPAMBANO YA KWELI NA DHATI YAANZIE ZANZIBAR ZEN TUHAMIE BARA MPAKA KIELEWEKE !
 
Viongozi hawajui kama watanzania wote ni ndugu, leo hii hata kwenye familia zetu kila mtu ana chama chake cha siasa anachokipenda, unapoanza kubagua watu kwa misingi ya vyama vyao, leo hii unaweza kukuta mke CCM mme CHADEMA, mme anaumia kuminywa kwa demokrasia mke anachekelea, anakenua tu meno mbele ya mme wake, kitakachotokea hapo ni kipigo cha mbwa mwizi kwa mke na kuvunjika kwa mahusiano.

Viongozi wanatakiwa watujengee umoja kwa kufuata misingi na utamaduni tuliojiwekea, wakupendana. Watanzania tunapendana sana bila kujali itikadi zetu ila leo hii tukianza kubaguana kiitikadi tutaleta mifarakano isiyo na msingi wowote. Mfano unazuia maandamano kwa UKAWA, CCM wanafanya maandamano na hakuna chochote wanachofanywa, unazuia mahafali kwa UKAWA wakati CCM wanafanya, Unazuia makongamano ya kujenga vyama ya UKAWA, wakati CCM wanakutana kukabidhiana madaraka. Unaruhusu mbunge wa upinzani aitwe msanii bungeni wakati wewe unataka uitwe mheshimiwa.
 
Back
Top Bottom