Chama cha ACT Wazalendo chasisitiza kutoshiriki uchaguzi wa Zanzibar
"ACT-Wazalendo
TAARIFA KWA UMMA:
Tumekuwa tukipokea simu za waandishi mbali mbali baada ya kauli ya jana ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),Jecha Salum Jecha kuwa hakuna chama kilichojitoa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika machi 20 mwaka huu
Msimamo wa ACT-Wazalendo ni kuwa hatutashiriki Uchaguzi huo kama ilivyoazimiwa katika kikao cha kamati kuu cha february 14 mwaka huu
Hatushiriki kwa kuwa tunaamini kuwa hakuna sababu ya kufanyika uchaguzi mwingine nje ya ule uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana
Taarifa hii ya kutoshiriki uchaguzi wa machi 20 mwaka huu imewasilishwa katika ofisi ya ZEC Zanzibar february 9 mwaka huu baada ya wao kututaka tuthibitishe kwa maandishi kama tutashiriki au la
Hivyo kauli ya Jecha kuwa hakuna chama kilichofuata utaratibu ni muendelezo mwingine wa kutaka kuhalalisha haramu kuwa halali kama walivyofanya katika kufuta uchaguzi wa Oktoba 25
Kwa kuthibitisha dhamira yetu hii ya kutoshiriki hivi karibuni kamati Maalum ya uongozi Zanzibar ilimsimamisha uanachama ndugu Khamis Idi Lila,aliyedhaminiwa na chama kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi uliofutwa kwa "Zengwe" hivyo hatuna mwanachama anayewania nafasi hiyo
Jecha amezungumzia Sheria ya Uchaguzi na wajibu wa mgombea aliyedhaminiwa na chama kuthibitisha ushiriki wake,huku akiacha kwa makusudi kuainisha udhamini huo ni katika uchaguzi gani
ACT-Wazalendo haijamdhamini mwanachama wake yeyote kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Machi 20 na hili lilipewa msisitizo katika kikao cha kamati kuu iliyofanyika february 14 na taarifa kutolewa kwa umma siku iliyofuata
Tunaomba wananchi wapuuze ulazimishaji huu wa ZEC kwa kutaka kuionesha dunia kuwa vyama vimeshiriki uchaguzi huo haramu
ACT wazalendo katika kikao chake cha kamati kuu iliazimia kuwa haitakuwa muhuri wa kuwasafisha wabakaji wa Demokrasia kwa kushiriki uchaguzi wa Machi 20
Abdallah Khamis
Afisa Habari
ACT Wazalendo
22/2/2016"
Source Zitto FB acc