Asante kwa tahadhari. Lakini ndugu yangu hapa hujawasaidia sana watanzania. Tatizo letu kubwa ni kukosa umakini katika kufikiri na kufanya maamuzi(yani hatupo critical). Unashauri twende dukani, ni sawa, hapa tutapunguza ukubwa tu wa tatizo, lakini madukani pia tunapigwa sana haya makorokocho. Kwanini hali ipo hivi?
1.Wengi si wadadisi, hajiulizi nataka ninunue nini wapi.Ukitaka nunua kitu iwe dukani ama online, jiulize muuzaji ni nani na ujiridhishe kwa kufanya tafiti.Sasa hata hivi ninavyoongea, ninaweza kutafuta mkopo wangu wa redio nikaufungasha vema nikapita nao mtaani sikosi hela ya kula. Lazima upate watu type hii wasio wadadisi. Mbaya zaidi hapo ukute kashakwepa kodi, hana risiti sahihi na hata kushitaki hawezi maana na yeye ni mhalifu.
2.Hachanganui bidhaa niitakayo ina thamani gani hasa ukilinganisha na ubora wake. Je, ninaweza kutoa lakini nane nikapata tv flat MPYA ya nchi 49? ya kampuni gani? Hapa wengi tunalizwa sana kwakuwa tunadhani inawezekana kumiliki kitu cha thamani na ubora mkubwa kwa bei cheee. Utashangaa mtu ana smartphone lakini hana hata wazo la kupitia na kujua hali za bidhaa anazotaka zipoje kimataifa, walau kumfungua ubongo asidanganywe.
Mimi ninakubali hatari ya kupigwa mtandaoni, lakini kwa kiasi kikubwa huchangiwa na ujinga wetu.
Asante sana kwa kuibua mada hii nyeti katika kipindi hiki ambacho kila mtu anaitafuta shilingi hata kwa kumpiga kabali jini mradi hela ipatikane.