Acheni kubagua Wazazi

Acheni kubagua Wazazi

blackcrow

Member
Joined
Sep 24, 2020
Posts
21
Reaction score
43
Unakuta umefunga shule umekuja nyumbani kwenu kula likizo unamkuta baba yako hayupo unamuuliza mama yako kuhusu baba yako anakuambia baba yako yupo kazini Unakaa hapo nyumbani kwenu mwezi mzima Muda wote upo na mama yako.

Mara likizo imeisha baba yako anakukuta uko chumbani kwako unapanga mabegi anakupatia shilingi Laki nane ya ada UnamuoMba hela ya matumizi anakupatia shilingi 80000 Ukamwambia haitoshi anakuambia maisha ni magumu unatoka hapo umenuna unakwenda sebuleni.

Mama yako anakuuliza kwa nini umenuna? Unamuhadihia anatoa shilingi 30000 anakupatia unafurahi unaingia facebook unaandika NANI KAMA MAMA? MAMA NI MUNGU WA PILI WA DUNIA Unajua kama baba yako baada ya kukulipia ada anakwenda kazini kwa miguu kwa sababu maisha ni magumu?

Unajua kama hiyo shilingi 30000 aliyokupatia Mama yako amepewa na Baba yako? Unajua kama umesoma kutoka Chekechea mpaka hapo ulipo. kwa jasho la Baba yako. ACHENI UBAGUZI WA WAZAZI JAMAN. KAMA UNAMPENDA BABA YAKO SEMA NAKUPENDA BABA.
 
Wababa wanapigana vita vya kimyakimya vingine visivyoonekana ila ndio hivyo kibongobongo juhudi za Mama ndio zinasemwa sana
 
Final mtoto ardhi yake ni kwa Baba
 
Ndiyo maisha, kama baba hujazaa mtoto hata mmoja wa Kike, jua uzeeni wewe wa kuumia tu. Watoto wa kiume wanajali mama zao tu. Wakike wanajali baba na mama zao; angalau kwa mabinti zetu tunapona
 
Nampenda Baba ile kinoma noma.
 
Back
Top Bottom