Acha wavurugane ili adui wa taifa hili aanguke. (the end of ccm)

Bagrameshi

Senior Member
Jun 22, 2012
131
43
Wawasalimu wana JF,
kwa watanzania wanaojua mambo kwa undani zaidi na wana mabadiliko halisi razima watakubaliana na mimi kuwa adui mkubwa wa maendeleo ya taifa letu ni CCM kwa sababu mara nyingi tumeona mtaji mkubwa wa hiki chama ni tabaka la ambao hawajafanikiwa kupata elimu inayostahili ya kuweza kuchambua mambo na kuchukua hatua sahihi.

Viongoizi wa chama hiki wamekuwa wakiungana kwa pamoja wakati wa uchahuzi na kutumia umoja wao kwa nguvu zote kuwalaghai watanzania maskini na ambao hawajabahatika kupata elimu stahiki ili waendelee kuwaweka madarakani. na hili siyo siri mtaji wa ccm umekuwa hasa mikoa ile ambayo kiwango cha watu waliosoma ni ndogo sana na hatimaye wanafanikiwa.

UMOJA WAO umekuwa ni siraha kubwa sana ambayo kwa awamu hii tunaona unaanza kuingiwa na kirusi amacho ninaamini unaweza kuwa mpango wa Mungu kutuondolea hili li DUBWASHA amabalo limeinyonya nchi yetu kwa miaka yote zaidi ya hamsini sasa. Mfano, ni wakati wa babeli baada ya watu kuzidi na kujawa na kiburi sana wakaona wajenge mnara ufike mbinguni lakini Mungu hakupenda upuuzi ule na alichokifanya ni kuchafua lugha zao wakashindwa kuelewana na hatimaye ule mpango wao ukafeli. kwa hiyo naona kwamba Hiki kirusi kinaweza kuwa siraha ya kuliondoa hili li DUBWASHA kwa jina la CCM.

shauku yangu ni kuona hiki kirusi kinawaparaganya ikiwezekana hata MAKAMU, WAZIRI MKUU, MAWAZILI NA WABUNGE WA CCM, VYOMBO VYA HABARI VYOTE wanaachana na huu mpango wa kushiriana na MKULU ili abaki na mwanae kipenzi. naamini hiki kirusi kitaendelea kufanya kazi kwa kasi kubwa sana kisiishie kwenye kamati ya madini tu.

Kwa hali hii ni wakati vyama vya upinzani kuunganisha nguvu kwa kiwango kikubwa saba waimarishe umoja wao kupitia UKAWA ikiwezekana hata vyama vingine vya upinzani vijiunge na ukawa kwa maandalizi ya 2020 kuingia madarakani kwa nguvu zote. naamani MUNGU YU NASI tunaiendea inchi ya ahadi.

TUSIOGOPE swala la tume kuendelea kuipendelea ccm nachokiamini pale mwanadamu anaona hakuna njia palepale MUNGU anasema kuna njia. hata kama ni Bahari ya shamu TUTAVUKA TU... amini usiamini NGOME ZA YERIKO ZINAENDA KUANGUKA.
MUBARIKIWE NA BWANA.
 
Back
Top Bottom