Acha dhambi mrudie Mungu wako kwa toba ya kweli

Acha dhambi mrudie Mungu wako kwa toba ya kweli

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,118
Reaction score
1,565
Isa 55:7 SUV
[7] Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.

Wito huu wa kuacha dhambi na kumrudia MUNGU sio wa Wayahudi peke yao, wito huu ni wa wanadamu wote, wanapaswa kuacha dhambi na kumrudia Mungu wao.

Zile tabia mbaya, Mungu hapendezwi nazo kwa Mwanadamu aliyemuumba mwenyewe, anataka ageuke na kutubu kweli, kuacha zile njia zake mbaya.

Matendo mabaya yasiyompendeza Mungu, kwa Mungu ni chukizo baya na yanamtenga mtu na Mungu wake, ule uhusiano mzuri na Mungu unatoweka kabisa kati ya mtu na Mungu.

Mungu wetu hapendi dhambi na ni mkali sana katika hilo, ila ni mwingi wa rehema, ukienda kwake ukatubu atakusamehe na kukufanya kuwa mtoto wake tena.

Zab 103:8 SUV
[8] BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.

Sisi kwa sisi tunaweza tusisameheane kwa yale tuliyokoseana, ila Mungu wetu ni wa tofauti, ukirudi kwake kwa imani na toba, na kuacha njia zako mbaya utapata msamaha wake.

Uzuri wa Mungu akishakusamehe habakishi kitu kwako, anakusamehe "kabisa" msamaha wake hauachi kiporo au mabaki ya hukumu, ukishaomba toba na kuacha njia zako mbaya, anakusamehe na unakuwa kiumbe kipya kwake.

Msamaha wake ni wa kweli, sivyo hivyo tu, ni wa kudumu, yaani hauna kikomo, labda uamue wewe kurudia maisha yako ya dhambi tena, hapo utakuwa umejifarakanisha mwenyewe na Yeye.

Mik 7:18-19 SUV
[18] Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hashiki hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema. [19] Atarejea na kutuhurumia; atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari.

Utaona ni jinsi gani Mungu alivyo mzuri sana katika maisha yetu, ni sisi huwa hatutaki kumsikiliza na kumfuata anavyotutaka, ndio maana tunakandamizwa vibaya na Shetani. Lakini tukiamua kuacha maisha ya dhambi, tutakuwa salama kabisa, tutapata uhuru wetu na kutoka katika utumwa wa dhambi.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom