Abdrahamani Kinana yupo Angola katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama vya ukombozi

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
0901e1c2eec322c0a3b8d6dad0855053.jpg

Sasa mda wote waligwaya nini hawa ccm kuweka haya hadharani?
Nadhani baada ya kubembelezwa mzee kakubali kurudi kazini!

=======

*TAARIFA*

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Abdrahamani Kinana yuko nchini Angola akiongoza ujumbe wa CCM katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama vya ukombozi wa kusini mwa Afrika( Front Line State parties).

Pia Ndugu Katibu Mkuu ameongoza Majadiliano na vyama Rafiki vilivyoshiriki Mkutano huo kikiwemo Chama Cha Kikomunisti Cha watu wa China .

Ujumbe wa CCM umejumuisha katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi( Ndg.Humphrey Polepole) Katibu wa Siasa na Uhusiano wa kimataifa(Ndg.Ngemela Lubinga) na watendaji wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Vyama Rafiki Vimepongeza CCM MPYA NA MWENENDO WAKE.
 
Vichwa kama hiki cha mleta mada ndio walioharibu UKAWA......nawaza huyu mleta mada anaweza kuwa Katibu itikadi na uenezi wa chama cha upinzani, eti hapo amepiga propaganada!
 
0901e1c2eec322c0a3b8d6dad0855053.jpg

Sasa mda wote waligwaya nini hawa ccm kuweka haya hadharani?
Nadhani baada ya kubembelezwa mzee kakubali kurudi kazini!
Acha mambo ya kudhania wewe.
CCM huwa hawafanyi mambo kwa mihemko mlishaambiwa kinana anapumzika baada ya kutoka kwenye matibabu,mkawa mnahemka wenyewe tu
 
Sikuzote ufipa tukiwaita vichwa vya wenda wazimu wanatukana ila nazani akili zao ni kama za mwenyekit wao
 
Ulikuwepo wakati wanambembeleza kurudi kazini?

Kazi tunayoiweza kwa sasa ni uwongo uwongo na udaku.
 
Back
Top Bottom