Jamaa aliona shemeji yake anachepuka, akaamua amtonye kaka yake(lakini sio wa mama/baba mmoja). Akamshauri kaka yake waweke mtego ili wamkamate live na huyo mwizi wa vitu vya wenzao.
Matokeo yake jamaa kaenda kamsimulia mkewe na kumwambia nduguye ndiye kamtonya.
Sasa shemeji kamdamkia shemejie leo asubuhi kamtukana vibaya matusi mengine hayafai kuandika ila miongoni mwao kamwambia shemejiye kwa sasa avae SKET, GAUNI, KANGA AU DELA kwani ni mbea kama mwanamke.
Jamaa leo hana raha, weekend yake mbaya kabisa wema umemponza.
Kwa wale mnaojua michepuko ya mashemeji zenu, kuweni makini kutoa infomation msije aibika.