Uanzishwaji wa viwanda wa Mwalimu nyerere ulifeli kwa sababu ya sera zilizotumika au "implementation program" ,
waliingiza siasa katika uendeshaji wa viwanda. mfano katika uanzishwaji wa viwanda hawakuangalia competion bali walitumia sera walizodhani ujamaa kugawanya viwanda nchi nzima, pili wakisema viwanda vinatengeneza ajira basi waliingiza watumishi viwandani si kwa ushindani na kuweka watumishi wengi kuliko uwezo wa kiwanda, mlolongo wa maamuzi uliathiri sana uendeshaji wa viwanda, mifumo ya kisiasa ilipewa kipaumbele kuliko mifumo ya kitaalamu.
Lazima utambue kuwa swala la kutumia kodi kulinda viwanda vya ndani ni la kitaalamu ila wazazi wetu walilichukulia kisiasa, mtu akisikia kuzuia bidhaa za nje basi analichukua hilo na kulifanya kisiasa. kuna mambo mengi yanayotakiwa kufanyika ikiwemo kuangalia ni bidhaa zipi kwa wakati gani na kwa viwango gani ziwekewe kodi ili kuchochea uzalishaji wa ndani