A-level au Diploma?

Unanikumbusha mbali kidogo wakat nakomaaa na bs na fundamental nkaambulia c,kwa ile pepa ilivokua wazi nlisema ngegonga A kali lakin wapi
 
ushauri wangu kama atapangiwa shule nzuri kama kibaha,mzumbe,ilboru,tabora mwache aende akasome alevel,ila kama atapangiwa shule za kawaida ni bora umpeleke chuo tu
 
Mbona Dogo anajiweza vizuri me nashauri aende advance
 
Mpeleke diploma, a level haitabiriki na haina mwenyewe,kama advance akasome shule za private tena zinazofanya vizuri sana kitaifa
 
Alevel ni building block kwa uwezo alionoa mpeleke Alevel itamsaidia hata akitaka kusoma kozi zingine baadae
 
Mpeleke akasome diploma hayo mengine yatafuata akishamaliza, tupo wengi ambao hata form 6 hatuijui.

Kule ni kupoteza muda na mikumbo kibao mwisho wa siku kama unavyosema hatatimiza malengo yake.
 
Asikudanganye mtu A-level ngumu... Ila mimi nasapoti aende advance coz ina heshima yake pia anakuwa na wide choice ya course ya kuchagua chuo.... Kwanza kabla hujafanya uamuzi mtathimini huyo dogo, he alifauli kisa ana bidii au kisa walimu walikuwa wana bidii? Kama ni walimu basi mpeleke tu diplo au advance ya private akakutane na walimu wenye bidii.... Me nawajua watu kibao nilisoma nao toka A-level walipasua One kali zaidi ya hiyo.... Wameenda A-level wametoka na 3 so fanya uamuzi bora
 
Kuna jamaa alipata points 09 olevel na alikuw ana passion ya udaktar vbaya mno
Shule alikuw anajiita Dr
Lakin advance imempotezea ndoto zake,sasa hv anasoma degree ya computer science IFM
Mpeleke diploma dogo awe na uhakika wa kutimiza ndoto yake
 
ushauri wangu kama atapangiwa shule nzuri kama kibaha,mzumbe,ilboru,tabora mwache aende akasome alevel,ila kama atapangiwa shule za kawaida ni bora umpeleke chuo tu
Mkuu hizo shule zilikuwa nzuri zamani sio kwa sasa
 
Mkuu hizo shule zilikuwa nzuri zamani sio kwa sasa

mkuu nalifahamu hilo,lakini kibaha,mzumbe,ilboru wako vizuri hauwezi kuzifananisha na tosa,pungu,azania nk.
na ata katika matokeo yao ya advance hauwez kukuta zero na hata div iv haziwezi kuzidi 4.
kwa upande mwingne hao madogo wanajielewa, kichwani wanauwezo wao binafsi wanafaulu bila ya mwalimu kuingia class.jaribu kutafuta matokeo ya advanc mwaka 2010 au 2011 uone madogo walivyokamua na kibaha wakatoa TO anaitwa muagachi A chacha,mzumbe wakatoa div 1=100,kibaha wakatoa 1=100.
 
Mpeleke dogo akapge clinical officer maana kama umesoma PCB,kufeli advance ni rahc Sana maana kufaulu kwake o,level kusikupe moyo mm naamini PCB ni combination ngumu kuliko zote duniani kwa sababu inamasomo mengi unaweza kusoma mpaka kichwa kikataka kupasuka utasoma PCB Kila somo linapractical,bado BAM(basic applied mathematics) and GS(general study) pia kama dogo anatoka family maskin,anaweza faulu vzur tu lakin mambo ya TCU wakamutupa education au faculty nyngne ambayo haikuwa moyoni na ikawa ngumu kubadli lakin akipga clinical officer baadae ni direct MD
 
Mpeleke dogo A Level mtafutie shule nzuri ya private ,kwa matokeo hayo dogo ana uwezo PCB atafaulu tu akikaza

Diploma ni route ndefu na usidhani akiingia ajirani ni rahisi kutoka kwenda kujiendeleza.Wengi wanaotoka inabidi waende kibishi na mtonyo unasitishwa so utasoma tu kama fresher

Then freshers atapata shida kwenye basic science pale,,dogo anaweza aende a level
 
Muulize anahtaj nn..kisha mpeleke,mbona cc tuko Advance na ni PCB na Mungu anatusaidia?...cha msingi ni kukomaa na kumwomba Mungu only
 
Kwa utaratibu wa TZ kama hajafanya A-Level kwenda MD sijui nimetoka kwenye system ya kusoma siku nyingi kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…