A Kiss From SeyShells.....

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
22,053
40,032
Kunjane! Dumela! !

Natumai mko poa wote, poleni mliokumbwa na changamoto mbali mbali.
Tukiwa tunajiandaa kuingia msimu wa mvua na baridi kwa huku johannersburg wiki yote hii tulikuwa na vikao ofisini kwetu na vilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi makao makuu huku South Africa Joberg. Hivo wiki yote hii kulikuwa na wafanyakazi wa nchi mbali mbali wa ofisi yetu wakihudhuria huo mkutano kwa siku tatu kisha wanarudi.
Sasa basi mie ndo mgeni nimeajiriwa mwaka huu hivo nikawa natambulishwa kwa hawa wafanyakazi wanaokuja kuwa nami ni mfanyakazi mwenzio. Sasa tangu jumatano mmoja wa wafanyakazi waliokuja alikuwa mkaka mmoja kutoka Sey Shells........ Hahahaaa najua mmewaza nini hehehee
Huyu kaka alikuwa siku zote hizi yuko vema tuu sasa leo wakati tunafunga mkutano tukawa tunaagana na hao wageni na blah blah na maongezi baada ya kikao kama mjuavyo watu wakitokaga kwenye vikao husimama kwenye korido na kuanza maongezi (mie huwa naona ni udaku tuu)
Basi huyu kaka aliyetoka Seychelles akawa kabaki kwenye chumba cha mkutano anafunga laptop yake na kuweka vizuri makabrasha yake wengine wote tukawa tumetawanyika niliporudi mezani kwangu nikagundua makabrasha yangu niliyaacha kule kwenye chumba cha mkutano. Nikawa narudi ili niyachukue niyaweke kwenye dawa to langu nitoke kurudi hotelini. (Bado sijapata nyumba ya kuishi) najua wengine mmepata swali jibu lake nalipiwa na ofisi ila ni kwa miezi 3 mwisho. Kwa kuwa kazi yenyewe ni ya kusafiri basi ofisi hapo ni shida kulipia hoteli maana ni mojawapo ya gharama za kampuni.

Ile nafungua mlango wa chumba cha mkutano yule kaka (Anaitwa Albert) alikuwa ndo ananyanyuka mezani nikamwambia Hi! I forgot my docs here nikachukua kabrasha zangu tukawa tunatoka basi akanisogelea kuniambia karibu Seychelles nikawa nanyoosha mkono wa kuagana nikashtuka jamaa kanisogelea na kunibusu kwenye shavu ikanibidi nijikaushe kuwa sikustuka nikajua vimeisha bado kanishikilia kunibusu na upande wa pili aaah nikabaki huyu kaka veeepee mbona salamu za kizungu kwa sanaa akati yeye muafrika kama mie. Nikatoa tena mkono kuagana hakushika basi tukaongozana mie nikaingia ofisini yeye akaondoka kurudi hotelini.
Hapo sasa na yeye kafikia hoteli hiyohiyo nilipofikia mimi maana niliposhuka mgahawani kupata chakula cha jioni nikamuona na yeye ndo anateremka kula. Wakaja wafanyakazi wengine pia wa nchi nyingine nao wako hoteli hiyohiyo tukaomba meza ya pamoja tukala pamoja. Wakati tunaondoka tukaanza kuagana tena haya jamani safari njema mfike salama muendako (kwa kiingereza) nikaanza kutoa mkono (shake hand) kuagana heee... hakuna aliyepokea mkono wangu wote wanakusogelea umbali wa sifuri na kukupiga busu la shavu la kulia na kushoto.
Nikajikuta najiuliza huu ndo utamaduni wa hii kampuni mie ndo sijui? Sikupata jibu ila najua ndani ya muda nitafahamu tuu.
Wakati huo lile busu la Albert lilishanisumbua kichwa nikijua Kasie amezimikiwa na Albert kumbe laah. Nimejicheka sana na kujiona daah nimewaza mawazo machafu tuu ya matusi matusi mapenzi mapenzi na krashi krashi.

Naomba Mola anisaidie niendelee kubana miguu hadi December maana ni kitambo sasa tangu nishikwe na ile huzuni nilipata kichefu chefu kila nikiwaza kuhusu biringanya mbili zinazoning'inia na kuipa karoti iliyo katikati nguvu ya kusimama. Usiniulize nini kilinipata hata nikutwe na hicho kichefu chefu.
Siku nikishukiwa na upako wa roho......... ntawaelezea kwa sasa .............
Bwana Note. (Usiku mwema kwa kitaliano najua haiandikwi hivyo ila inatamkwa hivyo).
Ciao.

Bibi Kasie.
 
hongera kwa kichefu chefu cha March mpaka December ila imekuwa haraka sana kukipata

ciao
 
hongera kwa kichefu chefu cha March mpaka December ila imekuwa haraka sana kukipata

ciao
Hahahahaaaa looh yaani kama umemaanisha hii maana niliyoipata saa hizi daah hahahahaa hapana bana sio kichefu chefu hikoo hahahahahaa
Yaani wakati naandika wala sikuwaza kama kunakuwaga na kichefu chefu hii ni kitu ingine kabisa. Halafu huo muda niliouweka kuanzia huu mwezi wa tatu hadi wa 12 daah ni muda wangu tuu japo kuna vitu nimevilenga ila sio hivo unavowaza wewe daah hahahahaaa.
Mwenzako mie niliwaza vibaya nikajikuta nimeumbuka kumbe Albert hana issue yoyote it was just a goodbye kiss from Seychelles.
Hahahahahaa
Kasie.
 
Back
Top Bottom