Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,273
- 4KSHARES
- PIN IT
All women should be concerned about their vaginal health. A healthy vagina is naturally acidic and contains rich quantities of beneficial bacteria that help fend off infections and maintain a normal pH level. A healthy vagina will also secrete small amounts of discharge to keep itself clean, much as saliva is produced to help cleanse your mouth. Any interference with these normal conditions, and you may face vaginal irritation or infection. Here’s how to keep your vagina healthy.
Wanawake tunatakiwa kuwa makini na afya ya vagina. Vagina yenye afya ina hali ya acidic na inahifadhi idadi ya bacterial ambao wanafaida kwetu kwakuwa wanatusaidia kupigana na maambukizi ya aina mbalimbali na pia kulinda hali ya alkaline pH. Vagina yenye afya nzuri pia itamwaga maji hii ni njia ya kujisafisha, kama mdomo unavyosafishwa na mate. Chochote kitakachoingiliana na hali hii ya vaginal itasababisha muasho na pia maambukizi.
1. Epukana na kusafisha vagina kwa kuloweka vagina kwenye maji, kwa muda mrefu (douching) wengine pia hutumia douching spray au sabuni, hii inaharibu pH levels na kuongeza mazingira ya acidic. Kawaida viginal inatakiwa kuwa na pH leves kati ya 3.8 - 4.5. Kama vaginal ina harufu kali na isiyofaa muone daktari, douching itapunguza harufu lakini sababu ya kuwepo kwa harufu hiyo inahitaji vipimo na dawa. Epukana na kutumia sabuni kali ndani ya uke na pia nje ya uke, hii pia inachangia kuchanganya kiwango cha pH.
2. Kula vyakula bora na vyenye afya, matunda na unywaji wa maji mengi ni siri ya kuwa na uke wenye afya. Yogurt na Cranberry juice pia vinasaida kulinda uke kutokana na yeast infection pia vitu hivyo huchangia tiba yake. Uke ukiwa mkavu sana, mazao ya soya yanasaidia kurekebisha hali hiyo.
3. Ni muhimu kutumia condomu wakati wa tendo la ndoa katika kulinda uke kutokana na magonjwa kama syphilis, gonorrhoea, genital warts, chlamydia, HIV na genital herpes. Magonjwa kama HIV na genital herpes hayana dawa mpaka sasa hivi, hata hivyo magonjwa kama HPV na genital warts yanaweza kusababisha cancer katika mwendelezo wake. Badilisha condom kutoka style moja kwenda nyingine, kwa mfano umeamua kufanya ora sex ukienda kwenye viginal or anal sex ni muhimu kubadili condom.
4. Jijengee utaratibu wa kumuona daktari wa wanawake (gynaecologist) angalau mara moja kila mwaka au kwa miaka miwili, usingoje mpaka upate tatizo.
5. Epuka kuwa na wapenzi wengi katika wakati mmoja, na pia kama umepata maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STD), hakikisha unamaliza tiba.
6. Epukana na matumizi ya Vaseline kama kilainishi, ni muhimu kumuandaa mpenzi wako au tumia lubricant jelly ambayo imepasishwa kwa matumizi ya binadamu. (kuna mkuu aliongea hili wiki iliyopita).
7. Usivae nguo za kubana sana, upe nafasi uke upate hewa, pichu za cotton ideally.
8. Ukiwa mwezini usikae muda mrefu bila kubadilisha taulo, hata kama flow siyo kubwa lakini baada ya masaa mawili/matatu ni muhimu kuweka taulo fresh. Kama ni wa kutumia toilet paper baada ya haja kubwa, jipanguse kutoka mbele kwenda nyuma, kuzuia maambukizi kwenye uke.