8 February 2016 , UKAWA kuweni makini sana na uchaguzi wa Meya wa Jiji la DAR ES SALAAM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,745
239,401
Wakuu natanguliza salamu , ukweli ni kwamba ccm inajuta vibaya mno kupoteza jiji la Dar es salaam . hili kila mtu anajua,

Lakini pamoja na wingi wa madiwani wa upinzani kuna taarifa zisizo rasmi kwamba ccm imeapa kupigana kufa na kupona kupigania roho yake , kwa njia halali au haramu , ni hatari tupu ! UKAWA Kuweni waangalifu sana ; nzi wangu amenidokeza kwamba mbinu zote zitajaribiwa ikiwemo vitisho ,

na kwamba UKAWA mkikaza na mkashikamana ushindi ni wenu maana siku zote namba hazidanganyi , kila la heri UKAWA

Nakala kwa Henry Kilewo .
 
Nasikia uchaguzi unarudiwa wa meya wa temeke & kinondoni, ni kutokana na hizi wilaya mpya.
 
Ukawa wanacheza total football wakati ccm wanacheza mbele kwa mbele
unajua kinachoisumbua ccm ni zabuni za jiji ikiwemo UDA , na nakuhakikishia kwenye haya mambo UKAWA ikitwaa jiji ( kama inavyotarajiwa na dunia nzima ) kuna watu watafungwa vifungo virefu sana .
 
Nasikia uchaguzi unarudiwa wa meya wa temeke & kinondoni, ni kutokana na hizi wilaya mpya.
hakuna pa kutokea mkuu , kuna watu visukari ni lazima vipande msimu huu , walipokuwa wanapanga uchaguzi hawakujua kama wataongeza wilaya ? na je kama wakiongeza wilaya sehemu nyingine miaka 4 ijayo uchaguzi wa meya utarudiwa tena ? hivi chama kizee kama ccm kinakubali ushauri wa Lizabon kweli ? hakika ccm imeishiwa pumzi .
 
Ukawa wanahitaji mipango thabiti na ya kufa kupona ili washinde jiji la Dar,vinginevyo CCM watajitangaza asubuhi na mapema.Ngoja niwape mfano wa kilichotokea kwenye uchaguzi wa meya wa jiji la Tanga.Kimsingi,madiwani wa Ukawa jijini Tanga ni wengi kuliko wa CCM,siku ya uchaguzu kura zilipigwa,na matokeo yakawa hivi CUF 21,CCM 18.Mkurugenzi(ambaye alikuwa msimamizi wa Uchaguzi akasoma matokeo kama yalivyo,watu wa Ukawa wakaanza kushangilia,Mkurugenzi akawatulizi ili amtangaze mshindi rasmi,mara PWAAAAA MEYA NI WA CCM!!!najua wengi mnaweza msiamini hiki ninachokisema lakini ndivyo ilivyokuwa,na polisi walikuwa wameshaandaliwa,wakaanza kuwathibiti madiwani wa Ukawa na kuwasweka rumande na Mkurugenzi akakimbia ofisi hadi leoo ninavyoandika sina uhakika kama amesharejea.CCM ni zaidi ya unavyoweza kuwafikiria......
 
Bila hata kufikiri sana kuna uwezekano wa CCM kushinda umeya wa JIJI?. Kwani meya wa JIJI si anachaguliwa na madiwani kutoka Halmashauri za manispaa tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni? Kama majority wa madiwani katika manispaa hizi ni wa UKAWA ina maana hata representatives wakakaoshiriki kwenye uchaguzi wa MEYA wa Jiji utakuwa automatically na wajumbe wengi kutoka UKAWA. Labda sasa iwe ndani ya UKAWA kuna watu watakaoamua kumpigia mgombea wa CCM kwa kuhongwa au kwa sababu nyingine yoyote. Nje ya scenario hii sioni kwa nini UKAWA wakose usingizi. " KUKU WA KWAKO ..... kwa nini uhangaike kutafuta mitego ya kumkamata"
 
Wamezoea kupindua wamepindua uchaguzi wa uraisi Tanganyika,Zanzibar,Tanga na Dar es salaam wafanye hivyo hivyo wanachokitengeneza wanakijuwa wenyewe wasije wakasema hawakuonywa
 
Ukawa wanahitaji mipango thabiti na ya kufa kupona ili washinde jiji la Dar,vinginevyo CCM watajitangaza asubuhi na mapema.Ngoja niwape mfano wa kilichotokea kwenye uchaguzi wa meya wa jiji la Tanga.Kimsingi,madiwani wa Ukawa jijini Tanga ni wengi kuliko wa CCM,siku ya uchaguzu kura zilipigwa,na matokeo yakawa hivi CUF 21,CCM 18.Mkurugenzi(ambaye alikuwa msimamizi wa Uchaguzi akasoma matokeo kama yalivyo,watu wa Ukawa wakaanza kushangilia,Mkurugenzi akawatulizi ili amtangaze mshindi rasmi,mara PWAAAAA MEYA NI WA CCM!!!najua wengi mnaweza msiamini hiki ninachokisema lakini ndivyo ilivyokuwa,na polisi walikuwa wameshaandaliwa,wakaanza kuwathibiti madiwani wa Ukawa na kuwasweka rumande na Mkurugenzi akakimbia ofisi hadi leoo ninavyoandika sina uhakika kama amesharejea.CCM ni zaidi ya unavyoweza kuwafikiria......
Mungu akulinde sana mkuu .
 
Bila hata kufikiri sana kuna uwezekano wa CCM kushinda umeya wa JIJI?. Kwani meya wa JIJI si anachaguliwa na madiwani kutoka Halmashauri za manispaa tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni? Kama majority wa madiwani katika manispaa hizi ni wa UKAWA ina maana hata representatives wakakaoshiriki kwenye uchaguzi wa MEYA wa Jiji utakuwa automatically na wajumbe wengi kutoka UKAWA. Labda sasa iwe ndani ya UKAWA kuna watu watakaoamua kumpigia mgombea wa CCM kwa kuhongwa au kwa sababu nyingine yoyote. Nje ya scenario hii sioni kwa nini UKAWA wakose usingizi. " KUKU WA KWAKO ..... kwa nini uhangaike kutafuta mitego ya kumkamata"
asante mkuu .
 
ukawa dareslam ipo juuuu hakuna kukonda wala kuhofia juu ya ufisadi wa maccm tunachukua jiji zima subiri muda ufike
 
Walitakiwa waanzie Morogoro kule ambapo walimdhalilisha mbunge kuwa haruhusiwi kuwa kwenye vikao vya madiwani viwili vilivyo kwenye jimbo lake!
 
Bila hata kufikiri sana kuna uwezekano wa CCM kushinda umeya wa JIJI?. Kwani meya wa JIJI si anachaguliwa na madiwani kutoka Halmashauri za manispaa tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni? Kama majority wa madiwani katika manispaa hizi ni wa UKAWA ina maana hata representatives wakakaoshiriki kwenye uchaguzi wa MEYA wa Jiji utakuwa automatically na wajumbe wengi kutoka UKAWA. Labda sasa iwe ndani ya UKAWA kuna watu watakaoamua kumpigia mgombea wa CCM kwa kuhongwa au kwa sababu nyingine yoyote. Nje ya scenario hii sioni kwa nini UKAWA wakose usingizi. " KUKU WA KWAKO ..... kwa nini uhangaike kutafuta mitego ya kumkamata"
Hawa ccm hawa aminiki hata kidogo ndugu yangu, ukisema ulalekidogo kumsubiria kuku aje bandani, kicheche anaweza akampitia.
 
Back
Top Bottom