4k ni mambo ya resolution nnavyojua mimi, na 3D ni dimensions za picha ama kuangalia picha ktk hali ya uhalisia, mfano ktk 3d movie mtu akiwa anapigwa shoka lets say usoni wewe mwangaliaji unaweza ukakwepa ukihisi unapigwa ww, kwa hyo mada yako naona 3d na 4k ni kama nyama na maharage ktk wali.
Kuuliza si ujinga..
Katika World Cup hii Sony wamesema kuwa watakuwa na moving camera za 4K ambazo zina uwezo mkubwa wa kutoa picha bora zaidi ya Camera za 3D.
Kwa wataalamu wa moving camera ni nini sifa za 4K na kuna tofauti gani na 3D aidha ni TV ya aina gani ambayo unaweza kuenjoy iwapo utapata matangazo ama movie iliyorekodiwa kwa kutumia mfumo wa 4K
Nimekupata mkuu,Unamaana gani kusema kuuliza si ujinga? Labda hujanielewa huo nimetoa mfano tu sio kukukejeli, ni nilimaanisha hivi unapoenda kununua Tv set mfano samsung zina features tofauti tofauti na bei pia ni tofauti hapa ndo mfano wangu unahusika sasa unaweza kununua 4k Tv isiwe 3d enabled, na pia unaweza nunua 4k Tv ikawa ni 3D capable, na pia zipo Hizi Hd tv za 1080p with no 3d technology, nadhani mfano wangu wa wali nyama na maharage umeuelewa sasa assume wali ndo Tv as tv halafu nyama ndo 4k technology na maharage ndo 3D technology kwa hyo unaweza kuagiza vyote kwa pamoja kwa urefu wa pesa yako tu.