2020 CCM ishakufa sasa dola ndo iko kazini

2020 CCM ishakufa sasa dola ndo iko kazini

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Posts
240
Reaction score
769
CCM kimekuwepo toka mwaka 1977 ni chama kilichotokana na muungano wa vyama viwili yaaani TANU na ASP chama hichi kilikubalika kwa wananchi na ni kwasababu nchii ilikuwa chini ya mfumo wa chama kimoja kilipata msusuko mkubwa mwaka 1984 kile kilichoitwa "kuchafuka kwa hali ya hewa zanzbar" hapo ndo kulipelekea mabadiliko ya katiba ya JMT nafasi ya rais wa zanzbar ikaondolewa kuwa makamo wa rais wa JMT.

Mwaka 1990 kulitokea kundi ndani ya ccm lililotambukuka kama G55 hawa waliidai tanganyika iliongozwa na kina njelu kusaka walijenga hoja kiasi kwamba serikali ilikubaliana nao hapo hayati baba wa taifa aliingilia kati na jambo hili lilimuathiri sana waziri mkuu wa wakati huo John malecela kumrithi mwinyi

Mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ukarejeshwa tena hapa ndipo CCM waliishi kama dola inayokubalika katka umma wa watanzania ccm ikawa imekubali mfumo wa vyama vingi kishingo upande na ni kutokana na mahitaji ya dunia vyama vya upinzani vikaanza kwa tabu sana kwanza hawakuwa na uhalali wa kisiasa wala wa kidola uchaguzi wa 1995 ccm ilipata wakati mgumu sana kutoka kwa Nccr mageuzi ya kina lyatonga mrema na mabere marando baada ya uchaguzi ccm ikaanza mkakati wa kuidhoofisha Nccr wakapandikiza chuki ikawa mapambano kati ya mwenyekiti na katibu wake mwshowe mzee mabere marando akanyosha mikono juu akamuacha mrema na NCCR uchaguzi wa 2000 chama cha wananchi cuf kikawa chama kikuu cha upinzani hapo kulekea uchaguzi wa 2005 CCM ikaanza kuidhibiti cuf upande wa bara I kafeli zanzbar unakumbuka aliyekuwa IGP mahita na hadaa ya visu na majambia kuhihusisha cuf na ugaidi mara chama cha waisilimu yote ni kutaka kisipate uhalali wa kisiasa uchaguzi wa 2005 ndo kipindi kuliibuka kundi lililojiita mtandao hili lilikuwepo toka 1995 lakini lilikuwa halijapata nguvu ndani ya ccm walikuwa watu wa propaganda sana hawa walijijenga ktk kupata uhalali wa kisiasa mgombea akawa Jakaya Mrisho Kikwete alishinda ushindi wa kimbunga wa zaidi ya asilimia 80 cuf bado kikaendelea kuwa chama kikuu cha upinzani kikafuatia cdm 2005 Hadi 2010

CUF kikaanza kikawekea mgogoro akaibuka kiongozi wa kambi rasmi bungeni Hamad rashid mbunge wa wawi cuf ikaangakia mgogoro wake mpaka uchaguzi mkuu wa 2010 huku cdm kukifukuta kwa kijana machachari mjenzi wa hoja ndugu Zuberi Kabwe Zitto kuchukua fomu ya uenyekiti ndani ya cdm ilibidi kina mzee mtei na makani waingilie kati na zzk kujitoa akamuacha mbowe agombee uchaguzi 2010 hapa ndipo cdm ilipopata nguvu ilivuna wabunge wengi kutoka bara na mgombea wake aliyekuwa katibu mkuu wake cdm Dkt wilbroad slaa kupunguza kura za Jakaya kutoka asilimia 80 mpaka 61 hapo ndipo cdm iliingia rasmi kwenye rada za ccm na dola kwanza kuhusishwa na ugaidi kupitia mkurugenzi wake wa usalama ndugu Wilfred lwakatare mwigulu alisema ana ushaidi kamili duniani Hadi mbinguni huku mgogoro wa kupandikiza ulioongozwa na profesa Kitila Mkumbo na mwigamba kwa kumuhadaa zitto kuhusu uenyekiti wa chama

Ishukuriwe idara ya ulinzi ya cdm ilifanya kazi yake wakafukuzwa cdm ikasonga mbele
Uchaguzi wa 2015 huu ndo uchaguzi uliokaribia kukiondoa ccm madarakani kama sio udhaifu wa katiba yetu Leo tungekuwa tunazungumzia historia ya ccm maana kwenye sanduku walipigwa bara na zanzbar dola ikatumika kuibakisha madarakani lakini ikakosa uhalali wa kisiasa kabisa hasa kwenye majiji muhimu kama dsm arusha mbeya na tanga kwa mara ya kwanza mgombea wa CCM alipata kura chini ya asilimia 60

Hapa ndipo tatizo lilipoanzia tunayoshuhudia sasa watu kubanwa kiuchumi kuminywa kwa demokrasia mpaka ununuzi wa viongozi wa upinzani hiii yote ccm inatafuta uhalali wa kisiasa waliokwisha upoteza sasa inatumika dola kuua upinzani hasa ununuzi wa wabunge migogoro ya kupandikiza kwenye vyama vya upinzani cdm na cuf kwa hiyo kiujumla ccm haina nguvu ya kushawishi tena zaidi ya kuitumia dola rejea chaguzi ndogo za kinondoni na siha na kwenye kata nyingi na hata ulioisha jana wa buyungu na kwenye baadhi ya kata sanduku la kura limefanywa kiini macho uporaji wa sasa ni wa wazi wazi kabisa

Hitimisho hii inayotumika sasa ndo mwisho wa ccm maana dola iko mbele ccm nyuma maanake ni dola itafika sehemu itaambatana na umma na hapa uhalali wa kisiasa utakuwa umeambatana na uhalali wa kidola ipo mifano mingi tu Tunisia Kenya Zimbabwe Egypt nk


Ndimi mwanagenzi dizzo mtawala
 
Uchambuzi makini. Fikilia mbinu ilyosupress magent wa upinzani kwenye sanduku la upigaji kura. Fikilia sana utagundua this was the last tact for the incumbent political party.

Katika maono ya tuliowengi tumekua tukiota siasa Safi katika nchi hii. Good democratic process ni msingi wa ustaarabu wa Nchi yoyote inayojari utawala bora. Tuwasihi watawala wafikilie Tanzania kwanza juu ya leo na kesho.mana Tanzania nzuri ya kesho hutengenezwa leo.
 
Yaani CCM wenyewe wanajua wananchi hawawataki , wamewachoka , hawakubaliki ndio maana wdnategemea dola policcm , tissccm , tumeccm hata Kauli zao zinathibitidha and I quote '' hata mkipigia kwingine ccm itashinda tu " Samia Suluhu . CCM mpaka wanawake ni majizi ya kura .
 
Hapana acha kupotosha, CCM ni CCM na Serikali ni Serikali zote zipo zinaendelea na majukumu yake kwa mujibu wa sharia. Zinajenga Nchi moja kila moja kwa majukumu yake. Kama ulisoma vizuri elimu ya Siasa tulikuwa tunafundishwa kuwa Serikali ni chombo cha utekelezaji wa majukumu ya Nchi.

Kazi ya chama ni kushika hatamu za uongozi kwa :- 1.Kuweka malengo, 2. Kusimamia utekelezaji 3. Kupima mafanikio. Kwa lugha za leo CCM inafanya Governance ya Serikali i.e.

Jamhuri, Muungano na za mitaa kupitia vyombo vyake vya utekelezaji katika ngazi mbalimbali kuanzia mashina, matawi, wadi/kata, jimbo ,wilaya ,mkoa na Taifa. CCM iko hai na inafanya kazi zake kwa weledi, ukitaka kujua angalia wananchi walivyoipa dhamana ya kuliongoza Taifa.
 
Uchambuzi makini. Fikilia mbinu ilyosupress magent wa upinzani kwenye sanduku la upigaji kura. Fikilia sana utagundua this was the last tact for the incumbent political party. Katika maono ya tuliowengi tumekua tukiota siasa Safi katika nchi hii. Good democratic process ni msingi wa ustaarabu wa Nchi yoyote inayojari utawala bora. Tuwasihi watawala wafikilie Tanzania kwanza juu ya leo na kesho.mana Tanzania nzuri ya kesho hutengenezwa leo.

Mwalimu nyerere alisema ili kuwe na maendeleo kwenye Taifa lazima kuwe na ARDHI, SIASA SAFI, UONGOZI BORA NA UTAWALA BORA
 
Back
Top Bottom