2017 umeisha ila Kero hii isivuke mwezi januari 2018

Fyafyafya

Member
Nov 30, 2017
53
187
Binafsi namkubari sana Raisi wetu John Pombe Joseph Magufuli kwa utendaji wake usiotia shaka.

Namkubari wani ana wasifu mzuri wa kuona kila kitu anachopenda kifanyike na hasinzii wala halali mpaka pale tu kitu hicho au jambo hilo limetekelezwa. Ni optimist.

Hapo nyuma tulitangaziwa kuwa Tv Chanel za ndani yaani ITV, STAR TV; EATV, AZAM TV; CHANNEL TEN, TV 1 n.k kuwa wananchi watakuwa wanaziangalia bila malipo yoyote yaani ni bure. Taarifa ilikuwa kuwa mwananchi atakuwa anarecharge king'amuzi chake kama anataka kuangalia channel za nje tu.

Kwa sasa hali ni tofauti kabisa. Tunashuhudia TBC pekee wakirusha matangazo yao bure bila malipo ila channel nyingine zote hawarushi mpaa ulipie!

Swali wananchi tunalojiuliza je kuna nini hapo katikati?

Maana mpaka sasa ivi
- TCRA wako kimya
- Waziri wa habari nae pia yuko kimya
- Raisi wetu mpendwa nae pi yuko kimya!

Mwenye kujua ukweli atujuze
 
Back
Top Bottom