Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
1. Ni mwaka ambao CCM itaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake
2. Watanzania watapewa ghiliba mpya kuwa sasa chama cha Mapinduzi kinarejeshwa kwenye misingi ya kuanzishwa kwake,
bila kuambiwa waliokiondoa kwenye misingi hiyo ni akina nani.
3. Watanzania wataambiwa kuwa chama kinaanza kujihusisha na
shida za watanzania, bila kuelezwa kwanini kazi hiyo hakikuifanya
muda wote wa miaka 40 ya mateso ya watanzania
4. Watanzania wataambiwa ni chama hiki kinaanza kuwa chama cha watu
kana kwamba miaka 40 hakikuwa chama watu na kimehadaa watanzania
5. Kudanganya watanzania kuwa sasa ndio chama kinaanza kuwa
cha watu, na kubeza kuwa waliokiongoza hiki chama ambao
wangali hai tangu awamu ya Mwinyi, Mkapa na Kikwete
hawakujali watu, na katu CCM ya 2017, inayojinasibu kuwa
itakuwa ya kipekee haitaweza kusema kuwa imeshiriki katika
kudumaza maisha ya watananzania kwa miaka 40 na Viongozi
wake wa sasa ni zao la mfumo ulioshindwa miaka 40
Huwa hatujiulizi, anayekudanganya leo alikuwa na aliyekudanganya jana na njia zao ni zile zile. Tushtuke