WanaJF,
Ninaandika waraka huu huku nikiwa na machungu mazito moyoni. Kwa mwaka 2012 niliingiza takribani kiasi cha shilingi millioni nne za kitanzania. Cha kusikitisha zaidi ya theluthi ya kipato changu nimekitumia katika michango ya sherehe za harusi, maulidi, kipaimara na nyinginezo. Nimesikitika sana. Hivyo kwa mwaka huu wa 2013 ninasikitika kuwajulisha sitachangia chochote katika mambo yanayohusiana na sherehe kama hizo. Ni ujinga na upotevu wa rasilimali wa bure. Kujuana isiwe tabu