:

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,976
Mwaka 1948 Wapalestina baada ya vita ya kujaribu kuiangamiza Israel, Wakimbizi 850,000 wa Kiyahudi walikimbia kwenda katika nchi za Morocco, Algeria, Tunisia, Libya, Egypt, Yemen, Syria, Lebanon, Iraq, Turkey. Wengi walihama baadaye kwenda Israeli na nchi nyingine za Ulaya na Marekani.

Kwa nini Wakimbizi wa Kiyahudi hawajulikani kuliko Wakimbizi wa Kipalestina? Ni kwa sababu wengi hawakubaki kuwa Wakimbizi baada ya Vita, mwaka 1949. Wengi wao waliamua kuacha nyumba zao, biashara zao, nk wakarudi Israeli baada ya vita bila kitu chochote. Ni wachache sana waliobaki mpaka leo!

Hebu tuangalie masuala mbalimbali yahusuyo wakimbizi wa pande zote mbili:

A. WAKIMBIZI WA KIYAHUDI.

Wakimbizi 650,000 wa Kiyahudi walikimbia toka mataifa ya Kiarabu na Kurudi Israel baada ya vita, wakimbizi 200,000 walihamia Marekani na Nchi za Ulaya!

Je, ni wakimbizi wangapi wa Kiyahudi walibaki katika nchi za Kiarabu baada ya 1948?
1. Iraq, walikuwepo 150,000, leo wako chini ya 10.
2. Algeria, walikuwepo 140,000, leo wako chini ya 50.
3. Egypt, walikuwepo 75,000, leo wako chini ya 20.
Hivyo hivyo, katika mataifa ya Kiarabu mengineyo.

Kuhusu wakimbizi wa Kipalestina. Ni wakimbizi wanaotunzwa na Umoja wa Mataifa kuliko wakimbizi wowote duniani.


B. WAKIMBIZI WA KIPALESTINA.
Baada ya vita ya kujaribu kuiangamiza Israel, mwaka 1948, wakimbizi 700,000 wa Kipalestina walikimbia Israel. Walisisitizwa na Nchi nyinginezo za Kiarabu kuondoka Israeli kwa kuwa Taifa hilo lilikuwa katika harakati za kuangamizwa na likishaangamizwa basi wangerudi. Waziri Mkuu wa Syria (1948 - 49) aitwaye Khalid Al-Azm aliwahi kusema kama ifuatavyo:

"Since 1948, We have been demanding the return of the refugees to their homes. But we ourselves are the ones who encouraged them to leave."

Mwaka 1949, Umoja wa Mataifa uliunda Mission iliyojulikana kama United Nations Relief and Works Agency (UNRWA) for the Palestinians. Hii ilikuwa ni taasisi kubwa iliyoundwa na iliyodumu kwa muda mrefu kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina tu. Mpaka mwaka 2017 taasisi hiyo ipo kwa ajili ya waliokuwa wakimbizi wa Kipalestina, Watoto wao na Wajukuu zao.

Bajeti kwa mwaka kwa UNRWA ni US$1,000,000,000/- ambapo US na European Union ndio wanaotoa fedha nyingi zaidi.


C. BAJETI KWA AJILI YA WAKIMBIZI WA KIYAHUDI?
Kwa upande wa Wakimbizi wa Kiyahudi, wao wanapata US$0. Wala hakuna msaada wowote ambao taifa la Israel linapata kwa ajili ya kusaidia wakimbizi hao kutoka UN au EU kama ilivyo kwa wale wa Kipalestina.


Muda mwingine unaposikia kuwa anazungumzia juu ya Wakimbizi wa Kipalestina, muulize pia azungumzie juu ya Wakimbizi wa Kiyahudi!

Karibuni kwa Mjadala!
 
Mods: Wekeni title: "Wakimbizi wa Kiyahudi vs Wakimbizi wa Kipalestina!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…