100k, 250k....

Manjeta

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
393
Reaction score
239
Jamani kuuliza si ujinga, hivi hii 100k (ikimaanisha laki moja) au 200k n.k hiyo 'k' kirefu chake nini? Na kwanini iitwe ivyo? Asili yake wapi? Na je kwanini isianzie 1k, 2k nakuendelea au kwanini isiwe 1L 'L'ikimaanisha 'Laki'??..naombeni kujuzwa maana hata mimi naandikaga tu 200k 400k nafata mkumbo tu...nijuzeni ili nikiulizwa namimi niweze kuidadavua.
 
K = Kilo == 1000,

100k == 100 * 1000 = 100,000
250k == 250 * 1000 = 250,000
 
Hongeza u..m...malizia na elufi ya kwanza kwenye jina la A..li kiba
 
We fata tu mana itakuwa kazi kukufahamisha hesabu ulizikimbia na c lazima kujua kila kitu
 

k = kilo (yaani mara elfu moja)
1k = 1000
100k = 100,000

Mkuu, elimu yako ni ya kiwango gani (msingi au sekondari)?
Hiyo ni namna ambayo hutumika kama vifupisho kupunguza idadi ya sifuri (katika namba).
Mfano mwingine ni 1m = 1,000,000 au 1b = 1,000,000,000
Kama ni ngumu kumeze we elewa tu hivyo hivyo.., 100K ni sawa na laki moja.

Pia 1L = 1000 mL (Hii ni kitu ingine kabisa). Hivyo L haiwezi ikamaanisha laki!
 
Apo nimekupta mkuu.
 

umechanganya madesa kidogo.

kifupi:

k Imetoholewa kutoka hesabu za ki itifaki za ki kompyuta kompyuta..

bits
bytes
kilobytes
megabytes
gigabytes
terabytes

sasa wanaposema k wanamaanisha kilo...(kutoka kilobytes),
ambapo ni wastani wa takribani 1000 bytes..(halisi ni 1024 bytes)..

ndy maana Y2K ni Year 2000....
 
Enheee haswaa nimekuelewa..asante sana.
 
Enheee haswaa nimekuelewa..asante sana.
Safi sana mleta uzi huu maana umewafanya na wengine wameelewa!kweli kuuliza siyo ujinga alafu hao wengine badala ya kuelekeza wanaponda wao ndy makanjanja
 
Safi sana mleta uzi huu maana umewafanya na wengine wameelewa!kweli kuuliza siyo ujinga alafu hao wengine badala ya kuelekeza wanaponda wao ndy makanjanja
Ha ha haaa kumbe hao ndo makanjanja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…