Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,003
Only 33 per cent of our total Government development expenditure in the past ten years has come from Outside in the form of loans or grants. This shows the degree to which we are relying first on our own resources and only looking outside when it is absolutely necessary, and when we are sure that we shall be able to repay on the due date. In fact, our 'self-reliance' in this respect has increased since the Arusha Declaration. In the last four financial years, an average of nearly 74 percent of our total development expenditure has come from internal resources, as against an average 56 percent over the previous six years. ..
It is possible, however, that in the future we may be able to allow ourselves to borrow from abroad a higher proportion of the money we spend on development. This is, of rouse, assuming that we can raise loans on acceptable terms and without political strings attached to them - condition which we will always insist upon in the futures, as in the past. But if we are able to do this, our development program will be able to proceed faster than otherwise, for finance is now a limiting factor for us- Nyerere in Ten Years after Independence.
My take:
so what is the problem?
Miafrika Ndivyo Tulivyo!!
Mwanakijiji:
Don't cherry pick what you want to say. Here are the facts 10 years later.
In a broadcast in December 1981 to mark 20th anniversary of Tanzania' independence JKN admitted: " We are poorer now than we were in 1972."
The following year, 1982, the annual level of foreign aids to Tanzania reached $600(almost 60% of the budget).
Wako katika kusukuma gurudumu la maendeleo.
Z10.
Zakumi hii ina maana 20 years of independence. Unaposema nina "cherry pick" ungeweza kuonesha kuwa alichosema Nyerere 10 years after independence nime kimisrepresent. Lakini unapokuja kuonesha what happened 10 years later unalazimisha tuhoji what happened?
Ilikuwaje miaka 10 baada ya Uhuru ambapo tulikuwa hatutegemei sana misaada ya kigeni tuliweza kufanya mambo mengi (soma hiyo hotuba yenyewe) halafu miaka kumi mingine mambo yamebadilika? Katika nukuu yako mwenyewe unathibitisha kuwa 10 years earlier we were better which was my point.
Kwa mtu yeyote anayejua historia ya dunia na Tanzania ndani ya miaka hiyo 10 uliyochagua wala hatapata shida kuelezea what happened. Lakini kile kilichotokea miaka hiyo hakiwezi kulinganishwa kwa kiasi chochote na kile kilichotokea miaka hii karibu thelathini iliyopita.
Ina maana huoni kuwa tulifanya vizuri na tulikuwa katika mwelekeo mzuri miaka ile 10 ya mwanzo ya Uhuru?
Mwanakijiji:
Historia ya 1971-1981 unaweza kuilemba kukupa execuses unazotaka uzisikie. Lakini ukweli wa mambo unabakia kuwa internal factors zinachukua sehemu kubwa ya matatizo hayo.
Na kama hizo internal factors tungeweza kuzifanyia kazi; tungekuwa mbali.
Naomba uzinyambulishe hizo internal factors ambazo tungeweza kuzifanyia kazi. Na uniambia kwa uhakika kuwa hakuna external factors zilichongia kuporomoka kwa uchumi wetu miaka hiyo ya sabini.
Zakumi,
Mkuu tafadhali usitake kupotosha watu.. Hata Marekani mwaka 1982 were poor kuliko mwaka 1972 kwani walikuwa na madeni hadi kooni inategemea wewe umeelewa vipi usemi huo..tumia facts na lugha inayoeleweka..
Kuna mdau anasema hivi Kuhusu Mwalimu Nyerere:
HE was the one that made Tz more dependent on aid than any other African country of his era and since.
HE sought and received aid from all Bretton Woods Institutions with impunity , indebting us nation for many years to come.
HE took part in a shameful deal to separate Biafra from the rest of Nigeria so that he could gain IMF support for all kinds of stupidity (largely corrupt activities) all in the name of Unity of the continent) Don't forget he was the architect and protector of the disfuntional OAU.
HE was a personal friend of Robert McNamara, the Director of The World Bank who gave him billions of USD (at the last count 16 billion USD) all of which has filtered away and never been accounted for? .......
And all Mwalimu had to do is ask rhetorical questions to distance himself from the mess and system and status quo that was funding and protecting him .
The West loved Nyerere. .......How is it that the capitalist coiuntries and institutions loved the saviour of "African Socialiism" a concept and phrase actually conceived by Nkrumah. Was he really working for Africans or for the West???
Companero,
Mkuu watasema sana lakini ukweli ni kwamba AID haina ubaya kama unajua unaifanyia nini.. Kama Nyerere alichukua mara 3 ya viongozi wa leo na akajenga miundombinu iliyopo, wakati hawa viongozi wote watatu wenye idea tofauti kwa miaka sawa na Nyerere ktk utawala wameshindwa hata kuongeza nguvu za Umeme, vyanzo vya maji. elimu bora (siku hizi kila shule inatumia vitabu vyake)..Afya bora, usafiri bora sijui hiyo mikopo tunayochukua leo inakwenda wapi..
Serikali haizalishi tena isipokuwa kutunga policies iweje tunashindwa hata kuujenga uwanja wa JKN uwe wa kimatifa na wa kileo kulingana na wakati..toka nguo mitumba, ferry boat mitumba, ndege mitumba, generator mitumba na yote inayotokana na mikopo..Hakuna chanzo chochote kilichojengwa toka mwinyi hadi Kikwete labda hizi generator na daraja la Mkapa.. hakuna hata kimoja zaidi ya ile waliyoikuta..
Hata ukitazama pale tulipofanikiwa kama Mawasiliano, mkuu wangu hakuna nchi inayoibiwa duniani kama Tanzania..Mitambo yote ni kuegesha yaani sio vyanzo ama ya kudumu kesho mkiwafukuza hawana noma kabisa wataondoka na furaha kubwa..Yaani mashirika ya mawasilino Tanzania yanatengeneza fedha kuliko migodi ya dhahabu au machimbo ya mafuta sema tu ni local monies..Hata Waarabu wenyewe wanatafuta uwekeshaji wa simu Tanzania..
Zakumi,
Alipewa nchi na nani? mkuu vipi lakini wewe ulitegemea nchi ambayo inatawaliwa na Queen wewe mmatumbi utayajua madeni yake wakati wewe mwenywe ndiye unaibiwa..
Again ulichozungumzia pale juu kuhusiana na 1971 through 1982 ni somo la Uchumi..kipimo kinachotumika hakina Tanzania wala Marekani..kumbuka tu unemployment ya Marekani ilifikia asilinia 21, hajawahi tokea ktk kipindi chochote kile.. Uchumi wa dunia nzima mwaka 1981 hadi 84 ulisababisha nchi zote za Kijamaa kukimbia mfumo huo kama hivi leo 2009 Ubepari unavyohangaika. Ukitazama uchumi wa Marekani unaweaza sema hali ya leo ni mbaya kiuchumi kuliko mwaka 1995..Kwa hiyo nachozungumzia hapa ni kipimo chako unachotumia.
Leo hii mkuu wangu sina kazi, kiuchumi hali yangu mbaya kuliko 1987 nilipokuwa nikifanya kibarua kwa dollar 5 kwa saa.. Hii haina maana maisha yangu ndi yameharibika kinoma..Re
Mkuu wangu hatubishani isipokuwa tunaelimishana kwa faida ya wote wanaosoma hapa..Hata kama kusingekuwepo na external factors, mipango yote ya 1971-1981 were doomed to fail kwa sababu moja kubwa tu waTanzania hawakuwa source ya maendeleo yao.
Huwezi kutumia pesa na kuomba omba na kukopa kujenga maendeleo bila ya wewe mwenyewe kuwa na shughuli za ku-sustain maendeleo hayo.
Zakumi,
Mkuu wangu hatubishani isipokuwa tunaelimishana kwa faida ya wote wanaosoma hapa..
Sijasema una spin, isipokuwa unapotosha kwa sababu unashindwa kuweka taarifa zako wazi..na hakuna sehemu nimezungumzia external wala internal factors.. hizi zipo kila nchi duniani iwe kwa maendeleo yao ama kuanguka kwao.. mimi sipo huko!
Nachozungumza mimi ni hali ya uchumi Tanzania nyakati mbili na vipimo ulivyotumia sijasema sababu kwani binafsi naamini kabisa kwamba bila mikopo ama omba omba tusingekuwa na muindombinu iliyojengwa..Na mara zote ktk uchumi unapojenga miundombinu ni kutokana na malengo ya kuongeza uzalishaji baadaye sio wakati unapojenga iwe ndio kipimo cha mauzo..Ila una create ajira, misingi na vyanzo vya uzalishaji.
Hata wewe mkuu wangu unapojenga nyumba (iwe guest house) pato au akiba yako haiwezi kuwa sawa na siku utakapo anza kupangisha nyumba hiyo..Ujenzi unaweza kukusukuma kuchukua mikopo na kuonekana omba omba lakini kwa mwenye kujua maana na soko la guesthouse atasema Zakumi ana akili kweli..
Tatizo langu ni ktk kutazama matumizi ya mikopo tuliyochukua. Nyerere alichukua mikopo na akaifanyia kazi kujenga misingi na vyazo vya uzalishaji tofauti na mikopo inayochukuliwa leo kukidhi mahitaji yasiyokuwa ya lazima na ndio maana tuna matatizo ya Umeme, maji, Afya, Elimu, Usafiri, na Uzalishaji wenyewe kwa sababu tumeshindwa kuweka misingi bora kulingana na ongezeko la watu na mahitaji yetu...
Nakuomba usome tena ile hotuba ya Mwalimu ambayo aliitoa baada ya Azimio la Arusha, nini malengo na misingi ya kukopa fedha kwani kukopa sio haramu ktk maendeleo ya Kiuchumi iwe kwa nchi ama mtu binafsi..
Bill Gates alikopa akawa omba omba na kila mwaka mikopo ilizidi ukubwa kulingana na mahitaji ya shirika lake hadi siku alipoanza kuzalisha na kupeleka mali yake sokoni ndipo tumeona maendeleo yake..
Binafsi naamini kabisa kwamba tuli fail kwa sababu ya mwongozo - SIASA ilokuwa ikituendesha pamoja na matatizo mengine ya nje.. ni somo kwetu lakini hatuwezi kujenga kambi ktk sababu zile kupindisha ukweli kwamba leo hii tunavuruga.. Obama amekabidhiwa nchi ina madeni ni jukumu lake kusoma alama na makosa yaliyopita kisiasa na Kiuchumi kuweza kusonga mbele lakini ni ujinga kutumia kipimo cha failure za Bush kujaribu kujenga hoja kwa nini atashindwa kufanikiwa..
Kiongozi bora ni yulke anayetazama beyond failure zilizopita na kuahidi wananchi kuwatoa ktk matatizo hayo na hata kuboresha nguzo za uchumi kwa kuweka misingi bora zaidi siyo kutumia matatizo yaliyopita kuonyesha udhaifu unaotokea ktk Utawala wake..
Kwa hiyo unafikiri Mkoloni aliacha misingi Bora!Kama kiongozi bora ni yule anayetazama beyond failure zilizopita na kuahidi wananchi kuwatoa ktk matatizo hayo na hata kuboresha nguzo za uchumi kwa kuweka misingi bora zaidi siyo kutumia matatizo yaliyopita kuonyesha udhaifu unaotokea ktk utawala wake basi TANZANIA HAIJAWAHI KUPATA KIONGOZI HUYO. Kama aliwahi kutokea PLEASE ENLIGHT ME.