Watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamepatiwa mafunzo kuhusu magonjwa sugu yasiyoambukiza mahala pa kazi pamoja na afya ya akili, leo tarehe 4 Julai, 2026 katika Ukumbi wa Hazina jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yameambatana na zoezi la upimaji wa afya kwa watumishi...