Miye sijui, walahi. Zamu yenu imefika. Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu. Mwafanya wenyewe, mkifanyiwa mnapiga nduru. Siye tulizoe kulia, kila siku kuumizwa na kulalamika.
Sasa tunataka zamu yenu ikifika tule kisinia kimoja. Walahi tutaumizana, kwetu haitakuwa mara ya kwanza. Mmetuua...