Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amesema kwa ukanda wa mikoa ya Kusini, yeye anabakia kuwa 'Simba'.
Nape ameyasema hayo leo, Aprili 13, 2025, wakati Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi na Mafunzo wa Ccm Taifa, Amos Makalla, akiendelea na ziara katika mikoa ya Kusini, Mtwara na Lindi.