Hospitali ya Taifa Muhimbili imeendelea kuwafikia watu mbalimbali wasiokuwa na uwezo ili kuwapatia huduma za matibabu, ikiwa ni kutimiza azma ya Mheshimiwa Rais katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ya kuhakikisha huduma za afya zinakuwa jumuishi, bora na zinazoweza kufikiwa na kila mwananchi...