Uwanja wa Ndege wa Arusha umeboreshwa kwa kuongeza muda wa huduma hadi saa 24, kutoka kufungwa saa 12 jioni. Njia ya kuruka na kutua ndege imeongezwa kutoka km 1.64 hadi km 1.84, huku eneo la maegesho ya magari likipanuliwa hadi takribani mita za mraba 15,000, hatua zinazoongeza uwezo wa uwanja...