Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,920
Siku ya jumanne nilipata msiba wa rafiki yangu ambae alifariki dunia ghafla
Jamaa yangu huyu alikuwa na maandalizi ya kufunga ndoa siku sio nyingi zijazo,kifo chake kilikuwa cha kustua sana na kilifanya watu washangae sana,mchana wa Jumatatu alikuwa ni mzima sana na ilipofika usiku ndipo alikutwa na mauti kwa kuugua kwa muda wa saa 1 tu
Katika zungumza yetu tukijadiliana hasa kuhusiana na kifo hicho ndipo kulizuka jambo ambalo lililonistua kidogo
Kulikuwa na wazee kadhaa ambao walidaio kuwa huenda kifo kile kilisababishwa na mchumba wa jamaa yangu yule ambae alikuwa ana mipango ya kuoana nae muda sio mrefu
Bahati nzuri aliyetarajia kuolewa nae namfahamu na ni rafiki yangu vizuri tu hivyo msiba ule ulinihusu kwa pande zote mbili,aliefariki na mfiwa pia
Kilichozuka kwenye mazungumzo yale ni kuwa wazee wale walidai kuwa mtoto anapozaliwa na kuanza kuota meno ya juu anapokuja kukua na kufikia muda wa kuingia kwenye mahusiano na kufanikiwa kuingia kwenye mahusiano serious ambayo yanaelekea ndoa au kuingia ndoani basi huyo aliyeingia nae ndoani au kuwa kwenye mipango ya kuoana nae hufa ghafla
Na sio huyo tu bali hata atakaefuata nae hufa na atakaepona ni yule wa tatu
Jambo hili kidogo lilinistua na ilibidi nihoji sana na wale wazee walinipa mifano kadhaa ili kuthibitisha kile walichokuwa wanakiongea,sasa sijui suala hili lina ukweli gani ila mfiwa akirudi nitajitahidi nitafute namna ya kumuuliza ili nianze kujua kuhusu hili,lakini kwa muda huu ni vyema tukaulizana hapa ili kama kujifunza tujifunze
Je suala hili lina ukweli gani waungwana?
Kama kuna ka ukweli kwa wale ambao bado hatujaoa tukawa na tahadhari hii ili tusijiingize kwenye hatari hii kwa kufanya uchunguzi wa kina
Ikumbukwe kuwa watu ambao wanaojiingiza kwenye mahusiano na aina hii ya watu hufa muda mfupi tuu na sio muda mrefu hivyo kama kuna mtu anaenda kufanya ka utafiti basi ni bora akajua hilo
Hebu tujuzane jamani Mtambuzi , ulishawahi kulisikia hili kwenye zile tafiti zako?
Kama kuna mwingine ana ujuzi au ufahamu wa hili tujuzane waungwana!

Last edited by a moderator: