Kwa Ushahidi ambao ulishaandaliwa na Kibatala&Co, Serikali ingetafuta pa kujificha, na isingepaona! Wala sio viongozi wa kidini waliosababisha aachiwe huru! Viongozi hawa wametumika tu ili kuwa kijisababu lakini Serikali imeogopa kuvuliwa nguo hadharani!
Mbowe ataonekana ana hatia kwa kulazimisha, atafungwa, na hatimaye ndipo mama yetu mwenye huruma atamsamehe labda kwenye sikukuu fulani hivi ya kitaifa!
Karl Peters aliyenunua nchi ya Tanganyika kwa Mangungo alikuwa Mjerumani! Huyu wa sasa aliyenunua Loliondo na sasa anataka kuongeza Ngorongoro ni Mwarabu! Historia haitakiacha kizazi hiki salama! Ila Mangungo wa sasa ni nani?
Hii ndio hali halisi ndani ya CCM kwa sasa! Wapo vipandevipande vinavyohasimiana! Mwendazake alikimaliza chama kabisa bila kujua. Tutaona na kusikia mengi bado!
Makamba alikuwa mpinzani mkubwa wa mradi huu tangu uanze. Kigezo chake kilikuqa ni uharibifu wa mazingira. Inapokuja sababu yoyote inayokwamisha mradi usiendelee, huwa simuamini Januari kabisa!
Kesi ya Mbowe ni mpango wa Mungu ili kufunua yote yaliyofunikwa. Kwa mfano mpaka kesi iishe tutakuwa tumejua idadi kubwa ya vikundi vya wale wanaoitwa "WASIOJULIKANA!" ambao hata Polisi wanasema hawawajui. Tumeanza kujua nani wanakamata watu, kuwaficha, na kuwaua!
Atakuwa mgombea dhaifu haijawahi kutokea. Kuna mpasuko mkubwa ndani ya CCM na kila siku anauongeza. Kwa vyovyote hatakubali Katiba mpya wala Tume huru ya uchaguzi. Ukatili wa Polisi atauongeza na itakuwa silaha yake kuu. Fikirieni ukombozi kwa njia nyingine lakini si hii ya demokrasia ya uchaguzi!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.