Thuli Mandonsela atangazwa mshindi wa tuzo ya Forbes Africa Person of The Year (POY2016)

Thuli Mandonsela atangazwa mshindi wa tuzo ya Forbes Africa Person of The Year (POY2016)

Status
Not open for further replies.
Kweeli

Kabisa! Bora wangehoji milioni kumi kumi za kusitisha ule mswada zilikwapuliwa wapi! Au zile pesa tulizochangia waathirika wa tetemeko zimeyeyukia wapi! Hivi kwanza walishapata jibu kuhusu uuzwaji holela wa nyumba za serikali? Au kile kivuko uchwara kilichonunuliwa kwa bei ya kufuru? Waambie bavicha waelewe bana!!waambie wahoji ni kwa nini Mh Lema amenyimwa dhamana kwa kosa la Kuongea alichokiota huku mahakama ikiwaachia kwa dhamana majangili yaliyoua Tembo 100!! Tatizo ni CCM!! Waambie Bavicha waelewe!
Nice comment!!!
 
Kama hii habari ni yakweli basi walio mpigia kura Raisi Magufuli wala wasife moyo kwa sababu hao watu wako kama MCC hufanya mambo kwa maslahi yao.
 
Aliyekuwa mlinzi wa maslahi ya umma nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela ametawazwa kuwa mtu mashuhuri zaidi wa Forbes wa mwaka 2016. Bi Madonsela aliwashinda marais watatu wa Afrika, raia mwenzake wa Afrika Kusini na watu wan chi ya Rwanda katika kushinda tuzo hiyo. Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake Ameenah Gurib wa Mauritania walikuwa wameteuliwa kushindania tuzo hiyo.

Mwingine ni mfanyabiashara wa Afrika Kusini Michiel le Roux ambaye ni mwanzilishi wa benki ya Capitec. Bi Madonsela, aliyetangazwa mshindi kwenye hafla iliyoandaliwa Nairobi Alhamisi jioni, amejulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi alipokuwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma Afrika Kusini.

Alihudumu kuanzia mwaka 2009 hadi 14 Oktoba mwaka huu, muhula wa miaka sita. Kipindi hicho, alimchunguza rais, akawachunguza wakuu wa polisi, maafisa wakuu serikalini na hata wanasiasa wa upinzani. Uchunguzi wake ulipelekea kusimamishwa kazi kwa mkuu wa polisi Bheki Cele mwaka 2011.

Aliwahi kumchunguza pia kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters Julius Malema ambaye mwishoni mwa kipindi chake, alimuunga mkono alipofanya uchunguzi kuhusu uhusiano wa Rais Jacob Zuma na familia tajiri ya Gupta. Alimchunguza pia Rais Zuma kuhusu ukarabati uliofanyiwa makao yake Nkandla. Bi Madonsela ni mama wa watoto wawili.

Alikuwa wakili na kiongozi wa vyama vya wafanyakazi wakati wa harakati za kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi. Huu ni mwaka wa sita kwa tuzo hiyo ya Forbes kwa mtu mashuhuri zaidi Afrika kutolewa.

Washindi wa awali ni: 2011 - Sanusi Lamido Sanusi, aliyekuwa wakati huo Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria. 2012 - James Mwangi, CEO wa Benki ya Equity, Kenya 2013 - Akinwumi Adesina, aliyekuwa wakati huo Waziri wa Kilimo Nigeria. 2014 - Aliko Dangote, mwenyekiti wa CEO wa kampuni ya Dangote Group, Nigeria. 2015 - Mohammed Dewji, CEO wa kampuni ya MeTL Group, Tanzania

Chanzo: BBC Swahili
 
Watanzania wataunganika na kuwa kitu kimoja katika kuleta maendeleo iwapo watagundua wanaongozwa na mtu aliyechaguliwa kihalali. tume mpya na katiba mpya vipewe kipaumbele.
 
tatizo tumezoea kudanganya TAKWIMU,mwalimu nyerere aliwahi kueleza vizuri sana juu ya UKWELI
 
Mwanasheria nguli wa Afrika Kusini na Mkurugenzi wa zamani wa Mashtaka Nchini Afrika Kusini, Bi. Thuli Madonsela ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Forbes Person of the Year 2016 na kuwaangusha wapinzani wake katika tuzo hiyo mbali ya kuzidiwa kura na Rais Magufuli ambaye pia alikuwa anawania tuzo hiyo maarufu duniani

Mpaka Forbes wanafunga zoezi la kupiga kura octoba 31, Rais magufuli alikuwa anaongoza kwa asilimia 84%.

Kwa mujibu wa kanuni wa tuzo hizo, mshindi wa tuzo hizo LAZIMA AKAICHUKUE HIYO TUZO YEYE MWENYEWE (PERSONALLY) na mwaka huu tuzo hiyo ilikuwa inafanyika nchini Kenya, Nov 17. Msimamo wa Rais Magufuli wa kupunguza safari za nje ndicho kilichosababisha aikose tuzo hiyo na kutangazwa kwa aliefuatia kwa kura, Bi. Thuli Madonsela.
 
Mumekuja na Utetezi Huo ni Uwongo Ulietukuka Mumeumbuka Mwenye Nyumba Hana Sifa.
 
Mwanasheria nguli wa Afrika Kusini na Mkurugenzi wa zamani wa Mashtaka Nchini Afrika Kusini, Bi. Thuli Madonsela ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Forbes Person of the Year 2016 na kuwaangusha wapinzani wake katika tuzo hiyo mbali ya kuzidiwa kura na Rais Magufuli ambaye pia alikuwa anawania tuzo hiyo maarufu duniani

Mpaka Forbes wanafunga zoezi la kupiga kura octoba 31, Rais magufuli alikuwa anaongoza kwa asilimia 84%.

Kwa mujibu wa kanuni wa tuzo hizo, mshindi wa tuzo hizo LAZIMA AKAICHUKUE HIYO TUZO YEYE MWENYEWE (PERSONALLY) na mwaka huu tuzo hiyo ilikuwa inafanyika nchini Kenya, Nov 17. Msimamo wa Rais Magufuli wa kupunguza safari za nje ndicho kilichosababisha aikose tuzo hiyo na kutangazwa kwa aliefuatia kwa kura, Bi. Thuli Madonsela.

Sababu ya Magufuli kukosa tuzo ni hizi hapa:

1.Kunyima RAIA wake uhuru wa kujieleza.
2.Kuwanyima wapinzani haki zao za kikatiba.
3.Kuingilia mihimili huru ya Bunge,Mahakama na Media.
4.Kuvunja sheria za nchi na Katiba kama alivyoapa kuilinda
 
Taarifa ni kwamba lile shindano lilikamilika na mh rais kaangukia pua au kalambishwa sskafu na Thuli Methusela wa Afrika kusini!

Ninachoshangaa ni kwamba wanalumumba walikwa wnadai anaongoza kwa 80% na wengine chini ya 10%. Je, nini kimetokea?

Tuliwaambia hizi tuzo zinamdharaulisha rais mkaktaa, ona sasa mtukufu rais wetu kaangukia pua!
 
Waliodanganya watu wakaacha kupiga kura kuwa ni za uongo, washerekehe sasa.

Ila watanzania wengi ni kweli wanaishi kwa kufata mikumbo, yaani hawana ile ya kujiuliza au kutaka kuhakikisha wao lisemwalo lolote hao wengi wanakubali tu. Inayoleta hii zaidi kwao ni uvivu na wivum
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom