15
Nyagani ni nani katika hii kesi?
SAA tatu asubuhi, askari wawili wakiwa na Land Rover kutoka kituo cha Mayamaya, waliwasili nyumbani kwa Mzee Chilyawanhu tayari kumkamata mzee huyo kutokana na kesi iliyofunguliwa kituoni kwao ikimkabili mzee huyo na ngariba Majimbi Uledi kwa kushirikiana...
14
Angewahishwa angeweza kupona
“MARINA, pole sana dada. Ninaitwa Jackson, mtoto wa Mazengo, sijui kama unanikumbuka?” Aliuliza kijana mwenye urefu wa wastani wakiwa wanasubiri taratibu baada ya kufikisha mwili wa marehemu kwenye chumba cha upasuaji ili kuchunguzwa.
“Jina siyo geni na hata...
13
Hamwezi kumzika mdogo wangu
MARINA aliwasili Mayamaya saa tisa mchana kwa gari la kukodi. Alimtaka dereva asitoke hadi atakapomruhusu ama kutoka naye. Alikuta ndugu, majirani na marafiki wakimalizia kula tayari kwa mazishi ya Celine.
Hali ile ilimkumbusha pia siku mama yake mzazi...
12
Lazima babu awajibike
MARINA alishituka. Alihisi amelala mahala asipopafahamu. Alizungusha macho kushoto kwake na kuona kitanda ambacho juu yake pia kulikuwa na mtu kalala. Kushoto kwake pia aliona mtu mwingine ambaye alikuwa ametundikiwa dripu. Hali ile pamoja na mashuka meupe ilimfanya...
11
Jikaze wewe ni msichana mkubwa
PALE nje walikaa kama dakika tano ambazo Marina aliziona kama saa, kisha mbunge akatoka. Akawakaribisha kwenye gari lake la kifahari. Ilionekana hakuwa amekuja na dereva wake. Mbunge huyo ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu mjini Dodoma wa maduka ya ya vifaa...
10
Kwenda hospitali ni lazima
AKIWA anaonekana kukata tamaa huku hasira zikiwa zimemjaa na kujilaumu kwa kuchelewa kuja Tanzania, Marina aliwafuata vijana waendesha bodaboda waliokuwa wakimsubiri kuwaeleza habari za mgonjwa aliyetaka wamsaidie kwenda hospitali kutoweka.
“Sijui nifanyeje...
9
Mila gani hizi zisizo na maana?
MARINA alitoka nje haraka akiwa amefura kwa hasira hadi pale alipokuwa ameketi babu yake akiendelea kula.
“Babu, mbona umefanya jambo nililokukataza sana… Imekuwaje mmemkeketa Celine?” Alihoji huku akitetemeka kwa hasira na kufuta machozi. Midomo ilikuwa...
8
Celine, are you sure?
GARI lile dogo sasa lilikuwa limeshaingia kijijini kwao, Mtakuja. Aliona nyumba ya babu yake ambaye ni mmoja wa wazee maarufu kijijini hapo mbele yao. Sasa alikumbuka jambo jingine muhimu alilosahau. Alishangaa kwamba safari yote kutoka Marekani, aliwaza kumwona Stella...
7
Huyu bwana anakufaa
MARINA alikumbuka siku iliyofuata, baada ya kufika kazini, aliitwa faragha na mama wa Kisomali. Hali ile ilimshangaza kiasi, kwani hata mahala walipokwenda kuongelea palikuwa maalumu, katika moja ya ofisi zake alikokuwa akifanyia mazungumzo na watu maalumu pia.
Kisha...
6
Mambo yako makubwa
ILIWACHUKUA dakika 40 wakiwa pale Mayamaya Madukani ambapo palikuwa pamebadilika sana; nyumba za kisasa na maduka yakiwa yameongezeka, ndipo wakaanza safari ya kuelekea kijijini kwao, Mtakuja, umbali wa takribani kilometa tatu kutoka hapo madukani.
“Shika njia ile pale...
5
Silazii damu mabwege
SIKU iliyofuata asubuhi saa 12, Stella alimchukua Marina hadi katika hoteli moja ya mama wa Kisomali ambako Marina sasa aligundua kwamba Stella alikuwa mhudumu wa hoteli hiyo ambayo pia ilikuwa na baa na tayari Marina alikuwa ameshamwombea kazi ya uhudumu.
“Mimi ni...
4
Safari ya Mayamaya
SAFARI ya kwenda Mayamaya ilipoanza, Marina akajikuta muda mwingi macho yake yakiangaza huku na kule kutazama mabadiliko ya mji wa Dodoma. Majengo marefu yalikuwa yamezidi kuongezeka.
Baada ya kupita Shule ya Wasichana ya Msalato ambako alipaswa kusoma kama mama yake...
3
Rudini kwa baba yenu
MARINA aliendelea kukumbuka namna alivyotoroka Mayamaya baada ya majogoo kuwika akiwa na mdogo wake huyo, Celine, siku ambayo alikuwa amepangiwa, yeye na mabinti wengine sita pale kijijini kupelekwa kwa ngariba ili kukeketwa baada ya jaribio la kwanza kutibuliwa na mama...
2
Sitaki yawakute yaliyonikuta
AKIWA bado amegubikwa na huzuni kutokana na maneno aliyoambiwa kwamba Stella hayuko hai, Marina aliamua siku yake ya pili kuwa Dodoma kuzunguka madukani ili kuangalia mabadiliko yaliyopo na kuona kama kuna zawadi zozote za ziada anazoweza kumchukulia mdogo wake...
TURUFU YA MWISHO
Aliporejea Tanzania baada ya kuwa nje kwa miaka saba, alikuwa na matumaini makubwa ya kumkuta mdogo wake Celine akiendelea vyema na masomo. Hakuamini baada ya kugundua alichofanyiwa Celine ambacho kilimuweka katika hatari ya kifo. Licha ya kupambana kumwokoa, akajikuta katikati...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.