Recent content by Nginana

  1. N

    Miaka 10 Kawe Barabara ni mitaro ya maji, Gwajima okoa jahazi

    Barabara karibu zote katika maeneo ya Oyster-bay, Masaki, Msasani na Mikocheni ambayo yako katika jimbo la Kawe zina lami. Barabara karibu zote katika majimbo ya Segerea, Ukonga na Kigamboni ambayo yalikuwa na wabunge wa CCM ni mbuvu; zimejaa mahandaki. Unasemaje hapo?
  2. N

    Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

    Kada Pascal, Hapa umepotosha kwa kiasi kikubwa. Sasa twende kimantiki (logical reasoning). Kwamba, barabara za mitaa ya jimbo la Kawe hazina lami kwa sababu mbunge wa eneo hilo anatoka chama cha upinzani na kwamba barabara za Ilala na Kinondoni zina lami kwa sababu wabunge wa hayo majimbo ni...
  3. N

    Uchaguzi 2020 NEC: Ni marufuku Wasimamizi wa Uchaguzi kufunga ofisi siku za kurudisha fomu na siku za uteuzi

    Tatizo ni kwamba kuna mamlaka yenye sauti zaidi juu ya hao maafisa wa uchaguzi kuliko mwenyekiti wa NEC na ambayo ina maslahi ya moja kwa moja na huu uchaguzi.
  4. N

    Japo yamesemwa mengi mazuri kuhusu Mkapa, kwa maoni yangu, maneno haya ya January Makamba ni one among the best kumhusu Benjamin William Mkapa

    Pascal, 1. Wewe mwenyewe umejifunza nini kutokana na hii? Mkapa taught me that prominence is good when it comes to you, not when you seek it. 2. Sioni mantiki yoyote ya wewe kuleta mada ya teuzi katika andiko lako hili. The only implication is you are so obsessed with "teuzi" that you feel...
  5. N

    Mapambano dhidi ya Covid-19 Tanzania na kwingineko Afrika: Watafiti na wanasayansi wetu mko wapi na munasemaje?

    Mathew Togolani Mndeme Hii thread yako ni fikirishi na inatoa elimu na kuuliza maswali ambayo yana umuhimu mkubwa sasa kuliko wakati mwingine wowote. Ili kufahamu ni kwa kiasi gani jamii ya Kitanzania inatambua wanasayansi na kuzingatia kazi zao za kitafiti, tuangalie upande mwingine wa...
  6. N

    CHADEMA badilikeni, kesi mahakamani hazitawapa kura. Mtaishia kumwaga lawama kwa kila ahusikaye na kesi zenu

    Anachotetea mtoa mada hapa, labda bila kufahamu, ni hii hali ya upendeleo katika mfumo wa utoaji haki nchini (differential treatment in the criminal justice system).
  7. N

    Kwa kauli hii, Rais Magufuli anakiri kuna mabaya yanafanyika chini ya utawala wake?

    Pascal, Karma; kama ilivyo imani zingine katika nguvu za giza - psychic powers - mfano, madai ya uwezo wa kusoma akili za watu (telepathy), madai ya kujua mambo yajayo (clairvoyance) na ramli (occult); ni imani ya ushirikina. Karma is a superstition. It is an irrational/unscientific...
  8. N

    Tanzania ni nchi huru, a Sovereign State, Mahakama zetu ni huru? Hizi ndizo hukumu zetu za haki, who the hell is Marekani kutuingilia? Je, tukubali?

    Pascal, Umetumia neno "sovereignty" (na mara nyingi unalitumia kimakosa) bila kutoa tafsiri yake kulingana na muktadha wa mada yako. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, "sovereignty" ni mamlaka ya serikali kutunga sheria zitakazotumika katika nchi ambayo iko katika mamlaka ya hiyo serikali. Hapa...
  9. N

    An overrated clout-chaser

    Nyani Ngabu Your argument is replete with logical fallacies. The so called party's tradition is little short of personal wishes of CCM's bigwigs and cannot in any way override the CCM constitution. The constitution protects (competitive) electoral democracy within the party. Membe is not in...
  10. N

    Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...

    Hili halina ubishi pamoja na kwamba safari hii haitatolewa sababu ya "zamu ya mwanamke". Ni vema Ndungai ajiandae kisaikolojia.
  11. N

    UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

    Pascal, Mchanganuo wako ni mzuri sana na kwa vile haya uliyoyainisha hapa hayafanyiki, haishangazi nchi itachelewa sana kupiga hatua ya maana kimaendeleo. Kama ulivyosema, serikali makini zinazojali maendeleo ya wananchi wake zinawekeza fedha kwenye miradi yenye multiplier effect kubwa kama...
  12. N

    UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

    Nadhani kuna tatizo kubwa zaidi kuliko uchaguzi wa vipaumbele hapa. Maintenance ya barabara mijini hasa uzibuaji wa mitaro ya maji kimsingi linapaswa kuwa zoezi endelevu (routine) ambalo halipaswi kushindanishwa na mradi mwingine wowote. Hili halikifanyiki na ndicho chanzo kikubwa cha mafuriko...
  13. N

    Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity

    Pascal, Umefanya jambo la maana sana kuambatanisha rejea zote muhimu (kama audio clips) ulizotumia kufanyia uchambuzi katika post yako hii. Hata hivyo, kimantiki kuna tatizo kwamba misingi uliyotumia kujengea hoja yako haiendani na hitimisho ulilofikia (your argument has true premises, but a...
  14. N

    Slaa anaamini katika nini? Kipenzi mbeba maono, msaliti wa umma au maslahi binafsi?

    Sawa. Ni maslahi binafsi zaidi ya itikadi na sera.
  15. N

    Neno na Manendo: Magufuli Umewaangusha Hawa 3(4) Usiache Kuwainua...

    Mzee Mwanakijiji, Kwanza, katika makala yako, kama unamaanisha "ng'ombe dume ambaye hajaasiwa", basi neno sahihi ni "fahali" na siyo "fahari". Pili, kwa maoni yangu, uchambuzi sahihi wa hili suala la hawa makada wa CCM kudukuliwa/kuwekwa hadharani mawasiliano yao binafsi ya simu na hatimaye...
Back
Top Bottom