PM huwa mgomvi sana saa nyingine. Tubaki tu kwenye mada leo. Kuwa mwanachama wa CCM haimaanishi una kubaliana na kila kitu au unaamini namna mambo yanavyokwenda ni sahihi ila kwa power dynamics zilivyo,basi tu,wenye nguvu wanaamua.
Nimekuja hapa kupongeza na kushukuru sana Mungu kwa kukuumba na kukupa uwezo mzuri sana lakini zaidi kukushukuru Dr. Mama Amon kwa kutumia vizuri uwezo wako na muda wako. Wewe ni mzalendo kweli kweli. Pamoja na kuipenda CCM naipenda Tanzania zaidi. Na andiko hili watalielewa zaidi wanaoipenda...
Huyu ndio Lema akiwa hajasoma upepo. Ndio maana kafuta tweet. Kipindi kile alikaa CANADA anawasoma akaja kuwaambia mlichotaka kusikia. Leo Tajiri Mbowe aliyelipia mkutano milioni 200+ na kutuhumiwa kwa rushwa anatakiwa kununuliwa gari kwa fedha za maskini kupitia michango kama ya Join the chain...
Ushauri mzuri Kaka. Ukweli ni kuwa hili jambo madhara yake ni makubwa kwenye ngazi za chini na huko mbeleni kwenye nafasi hiyo.
Ninaamini Dada Mkubwa angepitishwa na Chama bila huu utaratibu ila sijui yeye anajua nini so naishia kushangaa.
Namuombea Mungu ampe washauri wenye hekima na...
Vitengo hivyo kuwa chini ya Mwenyekiti ni demokrasia? Mnaposema fulani ana mamlaka makubwa huwa ni kwenye masuala ya kitaifa tu ila kwenye chama hamlioni? Safari ni ndefu kidogo.
They are both imperfect leaders. Wote si wakamilifu. Tubebe mazuri yao,tujifunze kwa makosa yao na madhaifu yao. Tuendelee mbele. Wote ni wazalendo kwa namna moja au nyingine.
Heshima yako Boss,nimeusoma huu uzi leo. Una maono ya mbali sana. Ni kama ulipanga haya matukio kupitia mawazo yako haya. Rais Samia ana kazi ngumu kidogo,aendelee kupambana kike,tunajifunza mengi.
Chawa wanafugwa na kuelekezwa.Wao sio wajinga ni maskini tu na njaa zao,wanajua kupambana na anayepambana na taasisi ya Urais ni kujimaliza. Wanajipanga ila bado ngumu sana wao kujaribu.
Na yeye ameamini wale ni kama Abdul kumbe wenyewe akili zao kwenye matumbo yao na vyeo na wakipata anayeshibisha tumbo zaidi hao hao chawa wanajigeuza kuwa maadui wa Rais. Asimamie yaliyo sahihi kupendwa atapendwa na watu sahihi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.